MAREKANI-OBAMA-TRUMP

Barack Obama: "Donald Trump hawezi kuwa rais wa Marekani"

Rais Barack Obama amshambulia Donald Trump mgombea urais wa chama cha Republican, akibaini kuwa "hajajiandaa vizuri" kuwa mrithi wake.
Rais Barack Obama amshambulia Donald Trump mgombea urais wa chama cha Republican, akibaini kuwa "hajajiandaa vizuri" kuwa mrithi wake. REUTERS/Joshua Roberts

Katika mkutano na waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Singapore, rais wa Marekani alipoulizwa kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya kampeni za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na utata kuhusu familia ya Khan, wazazi wa askari Muislamu wa Marekani aliyeuawa nchini Iraq, ambaye Donald Trump alimkashifu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Barack Obama, ambaye ameomba chama cha Republican kuacha kumuunga mkono, kila siku uzembe wa bilionea huyo unadhihirika.

Rais Obama amemshambulia mgombea huyo wa cham acha Republican, kwa madai ya kutokuwa na sifa stahiki kuwa rais wa Marekani.

Rais Obama amesema kwamba Trump amekuwa ni tofauti na wagombea waliopita wa chama cha Republican kama alivyo Mr Trump namna anavyotoa hukumu ama tabia zake za kuajabisha ambazo haziendani na mtu anayetarajiwa kuchukua madaraka makubwa na yenye nguvu kubwa zaidi katika dunia.

Mapema wiki hii, Richard Hanna mkazi wa mji wa New York alikuwa mwanachama wa kwanza wa chama cha Republican kutamka wazi kwamb atampigia kura mgombea urais kutoka chama cha Democrat Hillary Clinton.

Bw Hanna amemwita Donald Trump aibu ya taifa, wanachama wengine kutoka chama cha Republican wamejitenga kutomshabikia Trump ama hata kutomuunga mkono.

Kauli za Donald Trump, sera zake dhidi ya wanawake, masuala ya uhamiaji wa watu wasiokuwa na stakabadhi zinazotakiwa na Waislamu hayazingatiwi vilivyo na walio wengi kutoka upande wa chama cha Republican.