TAILAND-USALAMA-SIASA

Thailand: Katiba mpya yapitishwa, upinzani wadai kuwepo kwa shinikizo

Wafuasi wa upinzani wakipinga Katiba mpya ya ya utawala wa kijeshi baada ya matokeo ya kura ya maoni. Bangkok, Agosti 7, 2016.
Wafuasi wa upinzani wakipinga Katiba mpya ya ya utawala wa kijeshi baada ya matokeo ya kura ya maoni. Bangkok, Agosti 7, 2016. REUTERS/Kerek Wongsa

Matokeo ya mwisho yatatangazwa Jumatano wiki hii, lakini zoezi la uhesabuji tayari linaonyesha kwamba raia wa Thailand wamepitisha Katiba yao mpya kwa kura ya maoni (61.4% ya kura kwa jumla ya zaidi ya 94% ya kura zilizohesabiwa imepigia kura katiba hiyo).

Matangazo ya kibiashara

Rasimu ya Katiba hii iliandikwa na utawala wa kijeshi uliyochukua madaraka mwaka 2014 nchini Thailand.

Bila mshangao wowote, mkuu wa utawala huo wa kijeshi amekaribisha matokeo hayo. Jenerali Prayut Chan-ocha amesema kwa kura hiyo ya maoni imepigwa katika "uwazi" na kusema kuwa "anadharau" ukosoaji wa jumuiya ya kimataifa.

Upande wa upinzani wanasema kuwa kiongozi wa utawala wa kijeshi "hana sababu ya kujivunia" kwa ushindi huo. Viongozi wakuu vuguvugu la "Shati Nyekundu", vuguvugu la upinzani dhidi ya utawala wa kijeshi - wamekumbusha operesheni ya kamat kamata, ukandamizaji na ukosefu wa mjadala kabla ya kura ya maoni. "Kama katika utawala wowote wa udikteta ," wamebaini wapinzani ambao wanasema "wanaamini kwamba utawa siku moja utarejea mikononi mwa raia."

Lakini Katiba mpya ya Thailand inapitishwa na hatua zake zenye utata: Baraza la Seneti halitochaguliwa, lakini itateuliwa na utawala wa kijeshi uliopo madarakani na maafisa wa jeshi na polisi watateuliwa kwenye viti mbalimbali vya baraza hilo.