CHINA-AJALI

Ni mwaka mmoja sasa tangu bandari ya Tianjin iteketee kwa moto

Afisa wa Zima Moto akitembeakatika eneo kulikotokea mlipuko katika bandari ya Tianjin, huku kukiwa na magari yaliyoteketea kwa moto.
Afisa wa Zima Moto akitembeakatika eneo kulikotokea mlipuko katika bandari ya Tianjin, huku kukiwa na magari yaliyoteketea kwa moto. REUTERS/Stringer

"Bandari ya Tianjin, kituo cha ulimwengu cha uvumbuzi na mabadiliko." Tarehe 12 Agosti 2015, picha hii ambayo mji wa mwambao wa wakazi milioni 15 ulitaka kuwa nayo ilifutika muda mchache baada ya mji huu wa China kuteketea kwa moto, ikiwa ni moja ya majanga mabaya ya viwanda katika historia.

Matangazo ya kibiashara

Ghala lililokua lilihifadhi zaidi ya tani 3 000 za madawa ya kemikali lililipuka, na kusababisha vifo vya watu 165, ikiwa ni pamoja na maafisa 99 wa Zima Moto waliokua wametumwa kukabiliana na moto huo, na kuwajeruhi watu 800.

Kwa sasa katika kiwanda hiki kunaonekana tu mabaki ya majengo na majivu ya vitu bidhaa mbalimbali zilizokua zilhifadhiwa sehemu hiyo.

Thamani ya majengo na vifaa vilivyoteketea kwa moto ho ni sawa na Euro bilioni moja. Tangu wakati huo, serkali inajaribu kusahau tukio hilo baya kabisa kuwahi kutokea katika historia ya viwanda.

Mwaka mmoja baada ya kuhamishwa katika mji huo, sasa baadhi ya wakazi wameanza kurejea. "Ni wale ambao hawakua na uwezo wa kwenda mahali pengine. Serikali ilitupa maamuzi mawili: ama tupewe fedha kwa minajili ya kukarabati nyumba zetu, ama tuuze. Mimi niliamua kuuza nyumba yangu, " amesema Li Tian, ambaye alipoteza mali zake katika tukio hilo. " Watu wengi walipoteza maisha hapa," Li Tian ameongeza.