GABON-UCHAGUZI

Maelfu ya waandamanaji wakamatwa Gabon

Wafuasi wa Jean Ping wakpandishwa katika malori ya polisi, katika makao makuu ya mgombea wa upinzani, tarehe 1 Septemba katika mji wa Libreville.
Wafuasi wa Jean Ping wakpandishwa katika malori ya polisi, katika makao makuu ya mgombea wa upinzani, tarehe 1 Septemba katika mji wa Libreville. MARCO LONGARI / AFP

Vikosi vya usalama nchini vimewaweka mbaroni watu zaidi ya elfu moja wakati wa siku ya pili ya vurugu kufuatia uchaguzi wa rais. Watu watatu waliuawa katika mji mkuu wa Gabon, Libreville.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji waliokua wakiunga mkono kambi ya upinzani waliingia mitaani katika mji mkuu wa Gabon muda mfupi baada ya kutangazwa ushindi wa Ali Bongo Ondimba katika uchaguzi wa rais.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Ufaransa wametoa wito kwa kuwepo na uwazi zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi.

Waziri wa Mambo ya Ndani Pacome Moubelet Boubeya alisema Alhamisi wiki hii kwamba watu 800 walikamatwa katika mji wa Libreville na wengine 400 katika mikoa mingine.

Vikosi vya usalama vilitumwa baada ya jengo la Bunge kuchomwa moto na baada ya baadhi ya barabara kuu za mji kuzuiliwa.

Katika hotuba yake, Rais Bongo alisema: "Demokrasia hawezi kutumika kama bunge lake linashambuliwa."

Polisi ililitumia mabomu ya machozi kutawanya umati wa watu na kuwakamata watu waliokua wakitembea karibu na vifusi vya jengo la Bunge.