Viongozi wa nchi za EAC na utatuzi wa migogoro
Imechapishwa:
Sauti 09:59
Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi karibuni walikutana jiji Dar es Salaam na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo usalama na utatuzi wa migogoro katika kanda hiyo. Je viongozi hao wana nafasi gani katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa inayoendelea katika nchi hizo hususan Burundi na Sudani Kusini? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata uchambuzi wa kina kuhusu suala hilo.