AFRIKA KUSINI-ANC

Rais Zuma arejesha Euro nusu milioni katika hazina ya serikali

Makazi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika mji wa Nkandla.
Makazi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika mji wa Nkandla. REUTERS/Rogan Ward/Files

Nchini Afrika Kusini, Rais Jacob Zuma amelazimika kulipa sehemu ya fedha za umma zilizotumika kwa kukarabati makazi yake binafsi, katika mji wa Nkandla. Ofisi ya rais imethibitisha Jumatatu hii, Septemba 12 kwamba rais Zuma amerejesha Euro nusu milioni kama aalivyoagizwa na mahakama ya juu nchini Afrika Kusini. Hii ni moja ya kashfa zinazopaka tope utawala wake.

Matangazo ya kibiashara

Rais Zuma, hatimaye ameheshimu agizo la mahakama na kukubali kulipa karibu Euro nusu milioni kwa serikali. Hii ni sehemu ndogo ya fedha za umma zilizotumika kwakukarabati makazi yake binafsi na Mahakama ya Katiba alimuamuru kulipa pesa hiyo.

Katika utaratibu huu kuna mjumbe wa Jamhuri ambaye alihitimisha kuwa rais alijipa pesa kinyume cha sheria kwa kuendeleza shughuli za ukarabati wa makazi yake binafsi, kujenga bwawa la kuogelea na mambo mengine kwa pesa za umma.

Afisa huyo wa serikali alipendekeza kwamba Rais Zuma anatakiwa kulipa asilimia ya kuridhisha ya gharama, lakini ni baada tu ya vita vya kisheria ambapo Rais amekubali kulipa.

Kwa upande wa upinzani na mashirika ya kupambana na rushwa, ni ushindi dhidi ya ukatili. Katika matukio yote, kesi ya Nkandla, jina la makazi ya kifahari ya Zuma, imepaka tope muhula wa Rais Jacob Zuma na hivyo kupelekea chama chake cha ANC kushindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, mwezi Agosti uliyopita.