COTE D'IVOIRE-OBAMA

Barack Obama aondoa vikwazo dhidi ya Côte d'Ivoire

Kituo cha kusafishia mafuta karibu na mji wa Abidjan nchini Côte d'Ivoire.
Kituo cha kusafishia mafuta karibu na mji wa Abidjan nchini Côte d'Ivoire. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU

Jumatano wiki hii, Rais wa Marekani Barack Obama ameondoa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Côte d'Ivoire, zaidi ya miaka kumi iliyopita, wakati wa nchi hiyo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo vilichukuliwa na George W. Bush mwezi Februari 2006 dhidi ya viongozi kadhaa wa kisiasa wa Ivory Coast kwa kuzuia mchakato wa amani mwaka 2003. Wakati huo nchi hii ilikabiliwa na mgawanyiko wa kina tangu vita vya wenyewe vilivyosababishwa na uasi dhidi ya Rais Laurent Gbagbo mwaka 2002.

"Côte d'Ivoire imepata mafanikio makubwa katika kuimarisha taasisi zake kisiasa na kiuchumi, na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ambayo yaliitumbukiza katika vita," amesema Ned Bei, msemaji wa Baraza la usalama la kitaifa la Ikulu ya White House.

"Changamoto zimeendelea kusuhudiwa wakati ambapo nchi hii inakabiliwa na mageuzi magumu ya kilimo na ajira ambapo faida za ukuaji wa uchumi zinaonekana kwa watu wote wa Côte d'Ivoire," amesema Ned Bei.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliamua mwezi Aprili kuondoa vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya watu sita, ikiwa ni pamoja na Laurent Gbagbo, ambaye kwa sasa anasikilizwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Vikwazo hivi vya zamani vinavyodumu miaka kumi na mbili vilikua vinahusu vikwazo vya silaha, mali kuzuiliwa na kupigwa marufuku ya kusafiri kwenda nchi za kigeni.

Miaka mitano baada ya matukio haya mabaya, Côte d'Ivoire inapongezwa na baadhi kama mfano katika sekta ya ujenzi, ukuaji wake umeifanya nchi hiyo kuwa na uchumibora barani Afrika.