GABON-ALI BONGO

Mahakama ya Katiba yakataa kuwasili kwa wataalamu kutoka AU

Mahakama ya Katiba ya Gabon haitaki msaada wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa uchaguzi.
Mahakama ya Katiba ya Gabon haitaki msaada wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa uchaguzi. © (Photo : AFP)

Nchini Gabon, Mahakama ya Katiba itatoa uamuzi wake Ijumaa Septemba 23 juu kuthibitisha au la kuchaguyliwa kwa mara nyingine kwa Rais Ali Bongo. Upinzani unadai kuundwa kwa tume ya wataalam wa kufuatilia zoezi la kuhesbu upya kura katika mkoa wa Haut-Ogooué ambapo Ali Bongo alipata 95% ya kura na kuibuka mshindi.

Matangazo ya kibiashara

Kambi ya Jean Ping pia ilikua na matumaini ya kuwasili kwa wanasheria wa Umoja wa Afrika.Umoja wa Afrika, ambao ulikuwaukiwasiliana na serikali ya Libreville kwa kuwatuma wataalamu wake nchini Gabon, hatimaye hauna udhibiti juu ya mchakato huo.

"Majaji wa Mahakama ya Katiba watatoa uamuzi wao kwa niaba ya raia wa gabon. Wao walikula kiapo. Jambo ambalo hawafanyi wataalam wa kisheria wa Umoja wa Afrika, " amesema mwakilishi wa taasisi hiyo, akieleza kukataliwa kwa Umoja wa Afrika juu ya mchakato huo unaoendelea. Ameongeza kuwa hakutakuwa na zoezi la kuhesabu upya kura, lakini uchunguzi iapo uchaguzi huo haukugubikwa na kasoro za dhahiri. "Kazi ambayo kuja kwa wataalamu kutoka Umoja wa Afrika si muhimu, " amesema.

Umoja wa Afrika unasema, kwa upande wake, maelezo yalitumwa kwa serikali ya Libreville ili kueleza kazi ya wanasheria wake, bila mafanikio. "Mahakama haitaki timu yetu, " amesema mwakilishi wa Kiteng cha Amani na Usalama cha Umoj wa Afrika.

Jean-Remy Bantsantsa, mmoja wa wanasheria Jean Ping, amesema kuwa jambo muhimu ni kwamba tume ya wataalam inayowakilisha pande zote mbili inaweza kufuatilia zoezi la kuhesabu upya kura katika mko wa Haut-Ogooué. Lakini mwanasheria huyo ana wasiwasi hata hivyo.