Sehemu ya pili kuhusu hatua ya wakuu wa nchi za EAC kutotia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na EU, maarufu kama EPA
Imechapishwa: Imehaririwa:
Sauti 09:49
Kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunaendelea na mazungumzo yetu sehemu ya pili, kuhusu uamuzi wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutotia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya yao na ile ya umoja wa Ulaya, wataalamu wa masuala ya uchumi na hata baadhi ya wabunge wa bunge la Ulaya wanasema mkataba huu yafaa urekebishwe kwanza kabla ya kutiwa saini sababu hautakuwa na manufaa yoyote kwa viwanda vya ukanda.Tunaendelea na mahoano kati ya profesa Hamfrey Moshi, mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka Dar es Salaam, Tanzania.