Mahakama ya Katiba ya Gabon kutoa uamuzi Ijumaa

Jaji mwandishi akizungumza mbele ya Mahakama ya Katiba baada ya utaratibu uchunguzi, tarehe 22 Septemba mjini Libreville.
Jaji mwandishi akizungumza mbele ya Mahakama ya Katiba baada ya utaratibu uchunguzi, tarehe 22 Septemba mjini Libreville. RFI/Richard Riffonneau

Uamuzi wa Mahakama ya Katiba utakaohalalisha au la kuchaguliwa kwa mara nyingine ten kwa Ali Bongo, unatazamiwa kutolewa. Kimsingi, uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo Ijumaa tarehe 23 Septemba.

Matangazo ya kibiashara

Alhamisi usiku kulifanyika mjadala wa hadhara katika mahakama ya juu ya nchi hiyo. Kikao ambacho kinaashiria kumalizika kwa utaratibu wa uchunguzi.

Mawakili wa Rais Ali Bongo pamoja na wale wa mpinzani wake, Jean Ping, walikutana Alhamisi wiki hii katika Mahakama ya Katiba, na walisikilizwa mara ya kwanza kwa shauri la upingaji wa matokeo yaliyompa ushindi Rais Bongo.

Shauri hili lilianza kusikilizwa Alhamisi ya September 22, siku moja tu kabla ya muda wa mwisho wa siku 15 uliowekwa kikatiba kwa shauri hilo kuwa limetolewa uamuzi na Mahakama ya Katiba.

Rais Bongo alitangazwa mshindi baada ya uchaguzi wa Agosti 27, ambapo alishinda kwa idadi ndogo ya kura ambazo zilikuwa chini ya elfu 6, ushindi ambao ulizusha machafuko ya siku kadhaa kwa kupinga ushindi wake.

Upinzani ulipinga ushindi huo kwa madai ya udanganyifu September 8 mwaka huu, ambapo Ping mwanadiplomasia anayeheshimika kimataifa, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo, ambapo alifungua kesi kutaka kuhesabiwa upya kwa kura.

Mawakili wa Ping wamethibitisha kupokea wito wa mahakama, ambao uliwataka kufika mahakamni siku ya Alhamisi kuanza kusikiliza shauri lao.

Ping anataka kuhesabiwa upya kwa kura zote katikamkoa wa Haut-Ogoue, ngome ya rais Bongo, ambako alishinda kwa zaidi ya asilimia 95, eneo ambalo limeripotiwa kuwa watu waliojitokeza walikuwa ni zaidi ya asilimia 99.