Wimbi la Siasa

Chama cha Wananchi CUF chakumbwa na misukosuko

Sauti 09:57
Ibrahim Lipumba (kushoto)  akiwa na katibu mkuu wa chama  cha CUF Seif Shariff Hamad
Ibrahim Lipumba (kushoto) akiwa na katibu mkuu wa chama cha CUF Seif Shariff Hamad DR

Chama cha upinzani nchini Tanzania cha CUF kimeendelea kukumbwa na misukosuko ya kisiasa baada ya Mwenyekiti wake aliyewahi kuandika barua ya kujiuzulu Profesa Ibrahim Lipumba na baadaye kutaka kurejea katika kiti chake. Kama kwamba hiyo haitoshi chama hicho kimetangaza kumfuta kazi Lipumba huku yeye akijinasibu kuwa yeye ndiye mwenyekiti halali. Je hii ishara ya CUF kuparaganyika au kuimarika? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata mustakabali wa suala hilo.