MAREKANI-DONALD TRUMP

Trump ajaribu kujitetea kuhusu shutma za kutolipa kodi

Donald Trump hajalipa kodi kwa kipindi cha miaka 18. Taarifa hii iliyotolewa na gazeti la New York Times imesababisha utata nchini Marekani. Kulingana na waraka uliyopeperushwa na gazeti hilo, Donald Trump amesema kuwa alipoteza Dola milioni 916 mwaka 1995.

Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump.
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Donald na hasira. Ripoti ya taarifa ya mapato ya mwaka 1995, iliyotumwa na mtu ambaye hakutajwa jina kwa gazeti la New York Times inaonyesha kwamba baada ya vitega uchumi vyake kuanguka kiuchumi katika mji wa Atlantic City, mgombea urais wa chama cha Republican alisema kuwa alipoteza karibu Dola bilioni moja. Kutokana na hali hiyo, Donald Trump alisamehewa kutolipa kodi kwa kipindi cha miaka 18.

Ujanja huo si kosa, amesema mshauri wake, aliyekuwa Meya wa mji wa New York, Rudy Giuliani: "Ana wajibu, kama mmiliki wa kampuni, kutumia makato ya kodi yote ambayo yanapatikana kwa walipa kodi. Ukweli ni kwamba sheria zetu za kodi ndivyo zilivyo! ".

Donald Trump anaweza kuwa mjanja kwa ukwepaji wa kodi, lakini katika chama cha Democratic, Bernie Sanders ameonyesha upinzani wake: "Kwa kweli hivyo ndivyo mamilioni ya Wamarekani wanachanganyikiwa. Hata hivyo, Trump amesema "mimi nina mabilioni ya fedha na silipa kodi " lakini nyinyi mnapata dola 15 kwa saa moja na mnalipa kodi. "

Upande wa chama cha democratic wanatumia ufunuo huu uliyotolewa nagazeti la New York Times. "Hata kama mchakato huu ni halali, hii inabainisha kwamba biashara ya Donald Trump haistawi na kwa hakika washauri wake wa kodi washauri ni wenye ujuzi, lakini Wamarekani wanaomba mambo hayo yafanyike kwa uwazi," taarifa kutoka tume ya kampeni ya Clinton imesema. Donald Trump kwa upande wake ameahidi kulifungulia mashitaka gazeti la New York Times.