Maandamano yakithiri Cote d'Ivoire

Nchini Cote d'Ivoire, hali ya taharuki imeendelea kutanda kufuatia rasimu ya Katiba mpya iliyowasilishwa Bungeni ili ijadiliwe. Baada ya chama cha FPI, sasa ni zamu ya chama cha Lider kupinga rasimu ya Katiba mpya nchini humo. Chama cha Spika wa zamani wa Bunge, Mamadou Koulibaly, pia kimetowa wito kwa wafuasi wake kukusanya nje ya jengo la Bunge.

Hapa, rais wa Lider, Mamadou Koulibaly anaongea baada ya mkutano wa viongozi wa upinzani tarehe 18 Machi, 2015.
Hapa, rais wa Lider, Mamadou Koulibaly anaongea baada ya mkutano wa viongozi wa upinzani tarehe 18 Machi, 2015. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya upinzani havikubaliani na rasimu ya Katiba mpya nchini Cote d'Ivoire. Rasimu hii ya Katiba mpya tayari iliwasilishwa bungeni ili iweze kujadiliwa.

Lakini chama cha Lider tayari kimerusha rasimu hiyo ya katiba mpya kwenye mtandao, hata kama haujathibitisha ukweli wa hati hii na Ofisi ya Rais wa Cote D'Ivoire. Hati hii ambayo imethibitishwa na chama cha Mamadou Koulibaly, inapendekeza kuepo na nafasi ya Makamu wa Rais na Seneti.

Kuhusu Ibara ya 35, ambayo imekua ikizua mjadala mkubwa nchini humo imebadilishwa na Ibara ya 55. Ibara hii inasema kwamba "mgombea wa urais anapaswa kuwa alizaliwa na baba au mama ambao ni raia asilia wa Cote d'Ivoire. "

Kulinda "mambo ya ukoo wake "

Kwa upande wa chama cha Lider, wanasema Katiba inavyotakiwa na Alassane Ouattara ni mradi uliyoboreshwa ili kuruhusu rais kugombea tena atakapomaliza muhula wake wa pili, lakini pia ili kulinda "mambo ya ukoo wake".

"Katika mradi huu, Rais Ouattara amefaulu kukwepa baadhi ya pingamizi zikimkabili, kikomo kwa umri, kutoa nafasi kwa Jamhuri ya Tatu, " amesema Nathalie Yamb, afisa wa mawasiliano wa chama cha Lider.

Wiki chache kabla ya tarehe iliyopangwa kwa ajili ya kura ya maoni, maandamano yanaendelea. chama cha Mamadou Koulibaly, kwa upande wake, kimewataka wananchi wa Cote d'Ivoire kujielekez akwa wingi mbele ya jengo la Bunge Jumatano Oktoba 5 ili kupinga rasimu hiyo ya Katiba mpya.