COLOMBIA-FARC

Serikali ya Colombia na FARC kukutana tena kwa mazungumzo

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (katikati kushoto) akisabahiana na kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timochenko wakati wa kusaini makubaliano ya amani.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (katikati kushoto) akisabahiana na kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timochenko wakati wa kusaini makubaliano ya amani. Luis ACOSTA / AFP

Serikali ya Colombia na kundi la waasi la FARC wameanzisha tena mazungumzo ili kujaribu kutafuta njia muafaka ya kufikia makubaliano ya amani baada ya kura ya maoni iliyopigwa Jumapili iliyopita kupinga makubaliano na kundi hili la waasi.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya pande zote mbili kuwa na nia ya kukomesha mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano, Alvaro Uribe, rais wa zamani wa Cuba amekuwa akisisitiza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanatakiwa kurudiwa.

Rais wa Cuba Juan Manuel Santos amepanga kukutana na Alvaro Uribe Jumatano hii ili kuzungumzia suala hilo.

Hata hivyo serikali na kundi la waasi wanatazamiwa kukutana katika mji mkuu wa Cuba, Havana siku nne tu baada ya wananchi wananchi wa Cuba kupinga makubaliano ya amani kati ya pande hizo mbili..

Serikali ya Cuba imeunda tume itakayokutana Jumatano hii na wajumbe waliopiga kura ya hapana ili kuweza kuweka wazi vigezo ambavyo wangetilia maanani.