HAITI-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais na wa wabunge waahirishwa nchini Haiti

Nyumba zilizoharibiwa mjini Cayes, mji wa tatu  wa nchi ya Haitii, Jumatano hii, Oktoba 5, 2016, baada ya kimbunga Matthew.
Nyumba zilizoharibiwa mjini Cayes, mji wa tatu wa nchi ya Haitii, Jumatano hii, Oktoba 5, 2016, baada ya kimbunga Matthew. REUTERS/Andres Martinez Casares

Tume ya muda ya Uchaguzi nchini Haiti imetangaza kwamba uchaguzi wa urais na wa wabunge uliokua umepangwa kufanyika Jumapili, mwishoni mwa juma hili nchini Haiti umeahirishwa baada ya kimbunga Matthew kupiga katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Haiti, duru ya kwanza ya uchaguzi, uliofanyika mwaka 2015, ulifutwa kufuatia vurugu na udanganyifu mkubwa uliyojitikea katika uchaguzi huo. Viongozi wamepewa nafasi ya kutahmini uamuzi huo, baada ya kimbunga Matthew kupiga katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Haiti, Mwenyekiti wa Tume ya muda ya Uchaguzi (CEP) amesema, huku akiongeza kuwa majadiliano ymepangwa yanatarajiwa Oktoba 12 ili kutoa tarehe mpya kwa ajili ya uchaguzi.

Upepo wenye kasi za kilomita 220 kwa saa pamoja na mvua nyingi vilishuhudiwa katika pwani ya kusini mwa Haiti. Kulingana na makadirio ya muda, kimbuga Matthew kimesababisha watu saba kupoteza maisha . Na kwa sasa eneo la kaskazini magharibi la limeanza kuvamiwa.

Kwa sasa mvua inanyesha kwa wingi magharibi mwa nchi na barabara kuu, hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince na Léogâne, imeanza kukumbwa na mafuriko.

Katika mji mkuu, watu wamekua na wasiwasi kuhusu mto Grise. Mto huo umekua ukisababisha upepo mkali na maafisa wa Idara za dharura wameshindwa kuwakinaisha wakazi wa mji huo. Watu wengi wamekua wakijielekeza kwenye mto huo ili kushuhudia hali hiyo ya kutisha, huku wengine wakicheka wanaposukumwa na upepo mkali unaosababidshwa na mawimbi ya mto huo. Na wale ambao wanaishi katika nyumba hatari bado wanasita kuondoka katika maeneo hayo.

Mkoa unaoathirika zaidi nchini Haiti ni Grand Sud, hasa karibu na maeneo ya Jeremie na Les Cayes. Kiwango cha mafuriko na uharibifu ni kikubwa, lakini kwa sasa, ni vigumu kujua hali halisi katika eneo lote la kusini mwa nchi.

Bado mpaka sasa haijafahamika kiwango cha uharibifu wa kimbunga hicho nchini Haiti, lakini nyumba nyingi zimebomolewa, huku barabara zikiwa hazipitiki kutokana na miti iliyoanguka pamoja na mafuriko.