MAREKANI-SIASA

Baada ya mjadala kati ya Trump na Clinton, mgogoro waibuka katika chama cha Republican

Kwa maoni ya waangalizi, Donald Trump alijinyima fursa ya kupata wapiga kura wapya Jumapili Oktoba 9, 2016 katika mjadala na mshindane wake Hillary Clinton.
Kwa maoni ya waangalizi, Donald Trump alijinyima fursa ya kupata wapiga kura wapya Jumapili Oktoba 9, 2016 katika mjadala na mshindane wake Hillary Clinton. REUTERS/Shannon Stapleton

Hali ya sintofahamu imezuka katika chama cha Republican, siku moja tu baada ya mjadala mkali kati ya mgombea urais wa chama hicho Donald Trump na Hillary Clinton wa chama cha Democrat.

Matangazo ya kibiashara

Suala ambalo limekua gumzo leo nchini Marekani ni mgogoro wa ndani wa chama cha Republican. Karibu maafisa 50 wenye ushawishi mkubwa katika chama hicho wametangaza hadharani kwamba hawamuungi mkono mgombea wao. Vigogo kadhaa wa chama hicho pia wamebaini kwamba hawamuungi mono Bw Trump. Mitt Romney, Arnold Schwarzenegger na Condoleeza Rice ni miongoni mwa vigogo hao.

Wakati ambapo mkutano wa dharura kuhusu mgogoro huo umefanyika Jumatatu hii katika mji wa Capitol na viongozi wa Republican, baadhi wamebaini kwamba kwa kuimarisha kambi yake Jumapili usiku, Donald Trump alijinyima fursa ya kushinda uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Hali hii pia inaweza kuhatarisha viongozi waliochaguliwa kutoka chama cha Republican ambapo nafasi zao ziko hatarini, yaani Wawakilishi wote na theluthi moja ya wajumbe wa chama hiki katika baraza la Seneti. Spika wa Baraza la Wawakilishi, Paul Ryan, ametangaza kuwa 'hatoweza kufanya kampeni' kwa niaba ya Donald Trump, bila hata hivyo jujiondoa kumuunga mkono.

Chama hiki ambacho kwa sasa kinaonekana kufarikiana kitajaribu kupata wingi wa wajumbe katika Bunge na baraza la Seneti. Kwa yote hayo ukweli utajulikana Novemba 8.