CHAD-SIASA

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Chad akamatwa

Sera za kiuchumi za Rais wa Chad Idriss Deby Itno zinakosolewa na muungano wa vyama vya upinzani wa FONAC.
Sera za kiuchumi za Rais wa Chad Idriss Deby Itno zinakosolewa na muungano wa vyama vya upinzani wa FONAC. ISSOUF SANOGO / AFP

Nchini Chad, kiongozi wa chama cha upinzani cha PSF, Dinamou Daram amewekwa kizuizini tangu Ijumaa wiki iliyopita kwa kurusha tangazo linalowataka raia wa Chad kutolipa kodi.

Matangazo ya kibiashara

Dinamou Daram ni mwanachama wa muungano wa vyama vya upinzani unaopinga kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Idriss Deby baada ya uchaguzi wa urais uliopita wa mwezi Aprili.

Dinamou Daram alikamatwa baada ya kurushwa kwa matangazo ambayo yaliwataka raia wa Chad kuacha kulipa kodi na ushuru, kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa nchi na urasibu mbaya wa rasili mali ya nchi.

Dinamou Daram ambaye yuko chini ya ulinzi kwa kuchochea ukaidi dhidi ya serikali kwa mujibu wa Ofisi ya mashitaka,anatazamiwa kufikishwa mahakamani leo Jumatatu au kesho Jumanne, huku mgomo katika sekta ya umma ambao unaendelea ukiwa unaathiri uendeshwaji kazi wa mahakama. umma ambayo ulienda mahakama.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi na kutiwa saini na kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo, muungano unaojumuisha vyama ishirini vya upinzani (FONAC) umeomba Dinamou Daram kuachiliwa huru mara moja na kuwataka wananchi wa Chad kuacha kulipa kodi.