UTURUKI-URUSI-UCHUMI

Nishati: Urusi na Uturuki zasaini mradi wa Turkish Stream

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Istanbul, Oktoba 10, 2016.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Istanbul, Oktoba 10, 2016. REUTERS/Osman Orsal

Urusi na Uturuki wamesaini Jumatatu hii makubaliano juu ya utekelezaji wa mradi wa Turkish Stream kwa kusafirisha gesi ya Urusi barani Ulaya kupitia chini ya bahari Nyeusi, kwa mujibu wa waandishi wa habari AFP.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya zaidi ya saa moja na dakika arobaini za mazungumzo, viongozi wa Urusi Vladimir Putin na wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamekubaliana juu ya suala la mradi huu mkubwa wa nishati, kusahihisha maridhiano yao baada ya mgogoro mkubwa wa kidiplomasia uliyoibuka kufuatia uharibifu wa ndege ya kijeshi ya Urusi uliyotekelezwa na ndege ya kijeshi ya Uturuki ilipokua ikipaa kwenye mpaka wa Syria na Uturuki mwezi Novemba, 2015.

Mradi huu wa Turkish Stream ulizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2014 pamoja na kutelekezwa, baada ya kuibuka mgogoro wa Ukraine, kwa mradi uliyojulikana kwa jina la South Stream katika Bahari Nyeusi, uliofungwa na Umoja wa Ulaya.

Makubaliano yaliyofikiwa"yanaeleza ujenzi wa mabomba mawili ya gesi nchini ya bahari Nyeusi," Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gaz Prom, Alexei Miller amewaambia waandishi wa habarir. "Uwezo wa kila bomba ni mita za ujazo bilioni 15.75 za gesi kwa mwaka," amesema Bw Miller.

Mradi huu kati ya mawaziri wa nishati wa kila nchi, chini ya uangalizi wa Bw Putin na Erdogan umeafikiwa Jumatatu usiku masaa machache baada ya kuanza kwa kongamano kuu la 23 la Dunia kuhusu gesi linlofanyika mjini Istanbul, na wakati ambapo Kiongozi wa Urusi amekua akifanya ziara yake ya kwanza nchini Uturuki tangu kufanyika maridhiano ya nchi hizo mbili.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili ni wa tatu tangu Moscow na Ankara kukubaliana mwishoni mwa mwezi Juni kurejesha mahusiano yao, lakini ni mkutano wa kwanza kufanyika nchini Uturuki.