COTE D'IVOIRE-SIASA

Bunge laidhinisha mageuzi ya Katiba

Wabunge wa Cote d'Ivoire wakati ikiwasilishwa rasimu ya mageuzi ya Katiba Oktoba 5.
Wabunge wa Cote d'Ivoire wakati ikiwasilishwa rasimu ya mageuzi ya Katiba Oktoba 5. REUTERS/Luc Gnago

Bunge la Cote d'Ivoire lilipiga kura Jumanne hii katika neema ya mageuzi ya Katiba yaliyotakiwa na Rais Alassane Ouattara ili kuondoa hasa kifungu cha 'uraia wa Cote d'Ivoire' ambacho kilichangia kwa miaka mingi kuchochea machafuko na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2002-2003.

Matangazo ya kibiashara

Alassane Ouattara aliahidi mwaka jana wakati wa kampeni za kuchaguliwa kwake kwa mara nyingine tena kuwa kifungu kinachozua utata kuhusu uraia wa wagombea urais walio na wazazi wenye uraia wa Cote d'Ivoire, wakati ambapo nchi hiyo imekua ikiwapokea wahamiaji wengi.

Nakala hii mpya inafuta kifungu ambacho kiliwekwa na wapinzani wa rais wa sasa kwa kumzuia asiwezi kuwania katika uchaguzi uliopitaWatu wengi walitengwa katika siasa ya Cote d'Ivoire kutokana na kifungu hiki hasa wale kutoka kaskazini mwa nchi, ambapo familia nyingi zilizaana na jamii kutoka nchi jirani.

Kwa jumla ya wabunge 250, 239 walipiga kura katika neema ya mageuzi na ya Katiba sita walipinga. Katiba mpya sasa itawasilishwa kwa kura ya maoni tarehe 30 Oktoba.

Nakala hii pia inafuta kikomo cha umri wa miaka 75 kwa wagombea urais na inafanya rahisi mageuzi ya baadaye ya Katiba.

Baadhi ya wapinzani na asasi za kiraia walikosoa mageuzi hayo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa wadhifa wa makamu wa rais na Seneti ambao theluthi mbili ya wanachama watateuliwa na Mkuu wa Nchi.