COLOMBIA-FARC

Wananchi wa Colombia wamiminika mitaani

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos akizungumza kuhusu makubaliano ya kihistoria na FARC, Agosti 25, 2016 mjini Bogota.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos akizungumza kuhusu makubaliano ya kihistoria na FARC, Agosti 25, 2016 mjini Bogota. REUTERS/John Vizcaino

Mamia kwa maelfu ya watu nchini Colombia wanamiminika mitaani katika miji mbalimbali nchini humo ili kushinikiza kuzingatiwa kwa makubaliano yaliyoafikiwa na kusainiwa na serikali na kundi la waasi la FARC.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yamekuja baada ya muda mrefu wa mazungumzo lakini mapema mwezi huu wananchi wengi walipinga makubaliano hayo katika kura ya maoni, baada ya rais wa zamani Alvaro Uribe kuhamasisha wananchi wa Colombia kupiga kura ya “Hapana” kwa makubaliano hayo na kunddi la waas la FARC.

Mjini Bogota familia za wahanga wa mgogoro kati ya waasi hao na serikali walipewa maua meupe kama ishara ya amani.

Hivi karibuni Serikali ya Colombia na kundi la waasi la FARC walianzisha tena mazungumzo ili kujaribu kutafuta njia muafaka ya kufikia makubaliano ya amani baada ya kura ya maoni iliyopigwa Jumapili Oktoba 2 kupinga makubaliano na kundi hili la waasi.

Licha ya pande zote mbili kuwa na nia ya kukomesha mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano, Alvaro Uribe, rais wa zamani wa Cuba amekuwa akisisitiza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanatakiwa kurudiwa.

Bw Uribe amesema kunahitajika makubaliano mapya yatakayo wahusisha wananchi wote wa Colombia chini ya misingi ya sheria.

Kiongozi wa FARC Timochenko amesema kuwa atasita kujadili tena moja ya kifungu tata ambacho kinahusu kupunguzwa kwa adhabu ya kifungo kwa watakaokubali kuwa walikiuka haki za binadamu

Hata hivyo serikali na kundi la waasi wanatazamiwa kukutana katika mji mkuu wa Cuba, Havana siku nne tu baada ya wananchi wananchi wa Cuba kupinga makubaliano ya amani kati ya pande hizo mbili.