UFARANSA-SIASA

Kura za mchujo: wagombea watoa sera zao wakati wa mjadala wa kwanza

Wagombea saba katika kura za mchujo kutoka mrengo wa kulia katika mjadala, Oktoba 13, 2016.
Wagombea saba katika kura za mchujo kutoka mrengo wa kulia katika mjadala, Oktoba 13, 2016. REUTERS/Martin Bureau

Wagombea saba katika kura za mchujo kutoka mrengo wa kulia nchini Ufaransa wametoa misimamo yao wakati wa mjadala wa kwanza uliyofanyika kama sehemu ya kura za mchujo zilizopangwa kufanyika tarehe 20 na 27 Novemba kwa ajili ya uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao walimwaga sera zao wakati wa mjadala uliyorushwa kwenye runinga TF1 na RTL, katika mji wa Sain-Denis, nchini Ufaransa. Kila mmoja amezungumzia kuhusu uchumi.

Wagombea walioshiriki mjadala huo ni pamoja na Bruno Le Maire, Alain Juppé, Nathalie Kosciusko-Morizet, Nicolas Sarkozy, Jean-François Copé, Frédéric Poisson na François Fillon.

Kuhusu ukosefu wa ajira

François Fillon amesema: "Nitakapochaguliwa nitaweka kila kitu juu ya gharama ya chini ya Euro bilioni 40, katika ngazi zote za mshahara";

Bruno Le Maire amependekeza kubinafsisha Idara inayohuska na ajira. "dhidi ya ukosefu wa ajira, tumekua tukijitahidi kufanya mambo sawa. Je Idara inayohusika na ajira inatekeleza majukumu yake ipasavyo? Ni wazi hapana. ";

Jean-François Copé, sawa na Alain Juppe, anataka kupunguza marupurupu ya ajira na "kwenda mbali zaidi" katika kuleta mageuzi ya sheria ya kazi;

Alain Juppé amesema anaunga mkono marupurupu hayoyapunguzwe kwa 20% kwa mwaka mmoja na kisha 20% tena, baada ya miezi 18;

Nathalie Kosciusko-Morizet amesisitiza kuhusu ajira za kujitegemea ambazo zinajenga maisha ya "baadaye": anataka "kupunguza" ajira za kusaidiwa, kwa kuweka ya kazi kwa wafanyakazi wanaojitegemea.