MAREKANI-MICHELLE OBAMA

Michelle Obama amshambulia Donald Trump

Michelle Obama, mke wa Rais wa Marekani Barack Obama, Mei 8, 2014.
Michelle Obama, mke wa Rais wa Marekani Barack Obama, Mei 8, 2014. REUTERS/Yuri Gripas

Michelle Obama, mke wa rais wa Marekani, Barack Obama, amekosoa kauli ya Donald Trump ambayo amesema imewadhalalisha wanawake. Mgombea wa chama cha Republican anayetuhumiwa kuwanyanyasa kijinsia wanawake amesema analengwa na 'uongo wenye aibu' uliopangwa na mshindani wake kutoka chama cha Denocrat kupitia vyombo vya habari kwa minajili ya kumuangusha kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

"Katika chama chohote kile unachotetea, sawa na Democrat, Republican au mgombea binafsi, hakuna mwanamke anastahili kudhalilishwa kwa namna hii," amesema mke wa Rais wa Marekani Barack Obama, katika hotuba aliyoitoa Alhamisi wiki hii.

Michelle Obama ametoa hotuba hiyo kufuatia kauli chafu na yenye kejeli inayowadhalilisha wanawake iliyotolewa na Donald Trump mwaka 2005. Tangu maeneo yake hayo yawekwe wazi, Bw Trump ameshindwa kutuliza hali ya sintofahamu iliyosababishwa na kauli yake hiyo ndani ya chama chake pamoja na katika jamii nzima hasa wanawake nchini Marekani.

Hali hii ilianza kuwa mbaya zaidi tangu Jumatano bada ya wanawake kadhaa kutoa ushuhuda wa kunyanyaswa kimapenzi bila idhini yao. Kitendo kilichofanywa na Donald Trump.

"Sijawahi kukutana na watu hao. Wala sijui ni akina nani. huo ni uongo uliopangwa kabla ya uchaguzi," alisema Bw Trump Alhamisi hii katika hotuba yake kwa vijana katika mji wa Columbus, katika jimbo la Ohio, mashariki mwa Marekani.