DRC-MAZUNGUMZO

DRC: makubaliano ya kisiasa kati ya serikali na upinzani

Vital Kamerhe, rkiongozi wa chama cha UNC, na mwakilishi wa vyama vya upinzani katika mazungumzo, Septemba 1, 2016
Vital Kamerhe, rkiongozi wa chama cha UNC, na mwakilishi wa vyama vya upinzani katika mazungumzo, Septemba 1, 2016 JUNIOR D.KANNAH / AFP

Makubaliano ya kisiasa yalifikiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya vyama vinavyounga mkono serikali na baadhi ya vyama vya upinzani pamoja na baadhi ya mashirika ya kiraia. Makubaliano hayo yanatazamiwa kusainiwa Jumanne hii mjini Kinshasa na watu 300 walioshiriki katika mazungumzo, Msuluhishi wa Umoja wa Afrika Edem Kodjo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yalipitishwa katika kikao cha Jumatatu Oktoba 17. Lakini wajumbe katika mazungumzo hayo hawajapata nakala ya makubaliano hayo. Ni masuala yapi yaliyoafikiwa katika mazungumzo hayo?

■ Kalenda ya uchaguzi

Pointi ya kwanza ya makubaliano yaliyofikiwa na vyama vinavyounga mkono serikali na upinzani katika mazungumzo haya: hakuna tarehe kwa uchaguzi wa urais, wa wabunge na wa majimbo. Lakini tarehe ya kuwasilisha fomu za kugombea inajulikana. Ni Oktoba 30, 2017. Uchaguzi kwa upande wake utafanyika ndani ya muda wa miezi sita. Mwishoni mwa mwezi Aprili 2018, ndivyo wajumbe wa vyama vinavyunga mkono serikali na upinzani walivyoafikiana. Baadhi ya wajumbe wamekua wakijiuliza Jumatatu usiku wiki hii kama Tume ya Uchaguzi kweli itaheshimu tarehe hii mpya. Inapaswa kuhesimu, upinzani uliyoshiriki katika mazungumzo hayo umebaini. CENI ina majukumu yake, amesema mmoja wa wajumbe kutoka vyama vinavyounga mkono serikali.

■ Waziri mkuu kutoka chama cha upinzani

Pointi ya pili, Waziri Mkuu atateuliwa kutoka katika chama cha upinzani kiliyoshiriki katika mazungumzo. Hakuna maelezo kuhusu kugawana nyadhifa katika serikali ya umoja wa kitaifa. Kwa kukataa kutoa hisia kwamba ni makubaliano ya kugawana madaraka, wamesema wajumbe wa vyama vinavounga mkono serikali na wale wa upinzani katika mazungumzo hayo, serikali itaundwa ndani ya siku 21 baada ya kusainiwa mkataba.

■ Kamati ya ufuatiliaji

Pointi ya tatu, kamati ya ufuatiliaji itakutana mwezi mmoja baada ya kusainiwa kwa mkataba: wajumbe saba kutoka vyama vinavyounga mkono serikali, saba kutoka vyama wa upinzani na watatu kutoka vyama vya kiraia.

■ Hatma ya Joseph Kabila

Hatimaye, kuhusu hatma ya rais Joseph Kabila baada ya Desemba 19, inasemekana kuwa rais huyo ataendelea kusalia madarakani hadi atakapo tawazwa rais mwengine. Makubaliano hayo yanazungumzia tu juu ya kuzingatia kwa makini Katiba.

Hata hivyo vyama vya upinzani ambavyo vinajumuika katika muungano wa "Rassemblement" pamoja na baadhi ya mashirika ya kiraia ambayo yalisusia mazungumzo hayo yametoa wito wa kumiminika mitaani Jumatano Oktoba 19.

Hayo yakijiri Tume ya Uchaguzi (CENI) imeruhusiwa na Mahakama ya Katiba kuahirisha uchaguzi.

Hali ya wasi wasi na hofu ya kutokea machafuko nchini DR Congo imeendelea kutanda.