MAREKANI-TRUMP-SIASA

Mke wa Donald Trump, amtetea mumewe

Melania Trump, ajaribu kumtetea mumewe Donald Trump, baada ya tuhuma za kuwadhalilisha kingono wanawake.
Melania Trump, ajaribu kumtetea mumewe Donald Trump, baada ya tuhuma za kuwadhalilisha kingono wanawake. Fuente: Reuters.

Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump, amejitokeza na kumtetea mumewe kwamba tuhuma dhidi yake ni uzushi mtupu na ana muamini mumewe kuwa hawezi kukabiliwa na tuhuma kama hizo. 

Matangazo ya kibiashara

Melania Trump, amesema wanawake wanaomtuhumu mumewe kwa kuwadhalilisha kingono wamepangiliwa maneno kisiasa ili waweze kusema uongo kwa lengo la kumuangusha mumewe katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika Novemba 9. Bii Melania amesema akisisitiza kwamba mumewe ni "mwanamume mstaarabu".

Bii Melani amejitahidi kumtetea mumewe kwamba matamshi aliyoyatoa kwenye kanda ya video ya mwaka 2005 kuhusu wanawake hayakubaliki, hata kama amebaini kwamba hayaonyeshi mwanamume ambaye anamuamini.

Mgombea huyo wa chama cha Republican ana makosa ya kushiriki "mazungumzo ya wavulana faraghani" lakini alichochewa na mtangazaji wa runinga Billy Bush, Bi Trump amesema.

Bii Melania amemtwika lawama mtangazaji wa kipindi cha Access Hollywood cha runinga ya NBC, Billy Bush, kwamba licha ya “mumewe kuwa na makosa ya kushiriki mazungumzo na wanawake katika maeneo ya siri”, alihusika kwa kuchochea hali hiyo kwa lengo la kumuangusha kisiasa.

Itafahamika kwamba kanda hii ya video iliyotengenezwa mwaka 2005 na kurushwa kwenye runginga mbalimbali nchini Marekani imesababisha baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanasita au kuacha moja kwa moja kumuunga mkono Donald Trump.

Itafahamika pia kwamba Donald Trump katika kipindi hiki cha Access Hollywood cha NBC, alimwambia Billy Bush kwamba anaweza kujilazimisha kimapenzi kwa wanawake kwa sababu yeye ni mjanja kama nyota.