MAREKAN-CLINTON-TRUMP

Clinton na Trump wachuana kwa mara ya mwisho

Mdahalo wa tatu na wa mwisho kwa ajili ya uchaguzi wa urais nchini Marekani ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Nevada, Las Vegas Oktoba 19, 2016.
Mdahalo wa tatu na wa mwisho kwa ajili ya uchaguzi wa urais nchini Marekani ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Nevada, Las Vegas Oktoba 19, 2016. REUTERS/Mark Ralston/Pool

Mdahalo wa tatu na wa mwisho kwa ajili ya uchaguzi wa urais nchini Marekani ulifanyika Jumatano hii tarehe 19 Oktoba katika Chuo Kikuu cha Nevada, mjini Las Vegas. Hillary Clinton na Donald Trump walialikwa kuongea juu ya uhamiaji, haki za wanawake, silaha za kivita, sera za kigeni au uchumi.

Matangazo ya kibiashara

Ilikua pia nafasi kwa mgombea wa chama cha Republican kueleza kashfa ya ngono ambayo ilimlenga katika mdahalo uliyofanyika hivi karibuni.

Wagombea hawa wawili hawakupeana mkono kama katika mdahalo uliyotangulia, lakini katika mdahalo huu hapakua maneno ya kushambuliana kama ule uliyotangulia. Hali ambayo haikumzuila Donald Trump kukosoa mizania mibaya ya kugombea kwa Hillary Clinton.

■ Kivuli cha Putin

Hillary Clinton alimshtumu mshindani wake Donald trump kuwa 'mtumwa' wa Vladimir Putin. Rais wa Urusi 'anatamani kuwa na mtumwa badala ya kuwa rais wa Marekani' Bii Clinton amesema kwa kumjibu Donald Trump ambaye amekua akihakikisha kwamba Putin "hamheshimu" mke wa rais wa zamani wa Marekani Bill clinton.

Dakika chache baadaye, wagombea wawili walitupiana maeneno kuhusu taarifa zilizowekwa wazi na WikiLeaks, ambapo chama cha Democratic kinaona kwamba ni mbinu za Urusi kutaka kumpa umaarufu na nguvu Donald Trump.

■ Uhamiaji

Wakati wa mjadala huu wa mwisho, kwa mara nyingine tena, mgombea wa chama cha Republican aliwanyooshea kidole cha lawama wahamiaji haramu akibaini kwamba "wanawaletea zogo na vitendo vingine viovu". "Hatuna nchi kama hatuna mipaka. Hillary Clinton anataka kuwapa msamaha wahamiaji. Anataka mipaka iwe wazi. Tunapaswa kuzuia madawa ya kulevya. Kwa wakati huu tunapewa madawa ya kulevtya na wao wanapokea fedha. Hatuwezi kuwapa msamaha. "

Donald Trump pia alielezea nia yake ya kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico: "Tunahitaji ukuta. walinzi wa mipaka wanataka ukuta. Tunapaswa kuzuia madawa ya kulevya madawa ya kulevya. Tutadhibiti mipaka. Moja ya hatua zangu itakuwa kufukuza wafanyabiashara wa madawa ya kulevya. Hawa ni watu hatari. Tutawafukuza watu hawa. "

Hillary Clinton kwa upande wake ametoa wito kwa Wamarekani kuchukua uamuzi sahihi katika uchaguzi wa Novemba 8. "Nadhani ni sisi sote kuonyesha sisi ni nani na nini nchi yetu na kueleza wazi mategemeo yetu kwa Rais wetu mtarajiwa, vipi tunataka kuunganisha nchi yetu, badala ya kujenga mgawanyiko kati yetu, na badala yake tusherehekea utofauti wetu, tunasaidiana, na tunaifanya Marekani nchi kubwa zaidi. Marekani ni kubwa kwa sababu ni nzuri, " alisema Hillary Clinton.

■ Clinton azungumzia kuhusu heshima kwa wanawake

Kwa upande wake, mgombea wa chama cha Democratic alimshtumu kwa mara nyingine tena mshindani wake juu ya wanawake. "Donald anaamini kwamba kuwashusha wanawake kutamfanya kuwa maarufu."

Akijibu shutuma za kuwapapasa wanawake na kuwabusu bila idhni yao, Donald trump alinyooshea kidole cha lawama upande wa kambi ya upinzani, "wanataka kuwa maarufu, au ni timu yake mwenyewe" ambayo iliwashawishi wanawake wamtuhumu, alisema Bw Trump, akizungumzia Hillary Clinton.