UFILIPINO-CHINA-USHIRIKIANO

Duterte kufufua mahusiano na China

Marais wa Ufilipino (kushoto) na wa China,kukutana Alhamisi hii Oktoba 20, mjini Beijing.
Marais wa Ufilipino (kushoto) na wa China,kukutana Alhamisi hii Oktoba 20, mjini Beijing. REUTERS/Thomas Peter

Zaidi ya miezi mitatu iliyopita, Beijing na Manila walikuwa katika hali ya mvutano kwa sababu ya mzozo kwenye bahari ya China. Leo, Beijing inampkea rais wa Ufilipino. Alhamisi hii, Rodrigo Duterte atakutana na Rais wa China Xi Jinping na waziri Mkuu Li Keqiang.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufilipino amewashangaza wengi baada ya kujitenga na mshirika wake wa jadi Marekani kuanzisha uhusano na jirani yake.

"Ninasema, tuahirishe kwa wakati mwengine," Rais wa Ufilipino amesema akitabasamu katika mahojiano yaliyorushwa kwenye televisheni ya serikali ya China. "Hii ni changamoto muhimu kwa uongozi wangu kufungua uhusiano wa urafiki, ushirikiano na uboreshaji wa mahusiano kati ya nchi zetu mbili. Tunahitaji kuondoa kuondoa tofauti zetu. Nataka kuanzisha mahusiano ya nguvu kati yaUfilipino na China. Matumaini pekee ya kiuchumi Ufilipino ni China. Ili kuwa karibu nanyi: tunahitaji msaada wenu. "

Kauli hii ya Rais Dulerte imekaribishwa na viongozi wa China. Jumatano wiki hii, Hua Chunying, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, alikaribisha hoja kuhusu azimio la mgogoro 'kwa njia ya mashauriano na mazungumzo.'

Mikataba kadhaa

Ufilipino ni moja ya washirika waaminifu wa Washington katika bara la Asia. Nchi hizi zinaungana kwa mkataba wa ulinzi kwa nchi zote mbili. Lakini tangua mkataba huo uanze kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Juni, Rodrigo Duterte amekua akitumia muda wake kwa kugeuza sera za kigeni za nchi yake ili kurejea kuungana na China na Urusi. Serikali ya Ufilipino iliikosoa mara kadhaa Washington na Rais Barack Obama na kuomba isitishe doria ya pamoja na Marekani katika kwenye bahari ya China na kusem aikisisitiza mara kwa mara kwamba kutakuwa namazoezi ya kijeshi ya pamoja na Marekani.

Rais Ufilipino na wafanyabiashara 300 katika ujumbe wake wanasafiri China na mikataba kadhaa ya ushirikiano, na kuwa na matumani kwamba ndizi, maembe na mananasi vitavuka tena mpaka wa China kuingia Ufilipino.