UBELGIJI-CANADA-USHIRIKIANO

Ceta: pande kutoka Ubelgiji zafikia makubaliano kati yao

Waziri mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel (kushoto) akiwa na waziri wake wa mambo ya nje, Didier Reynders, 27 October 2016.
Waziri mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel (kushoto) akiwa na waziri wake wa mambo ya nje, Didier Reynders, 27 October 2016. REUTERS/Yves Herman

Waziri akiwa pia Rais wa jimbo la Wallonia, Paul Magnette amesema kwamba madai yake wamesikilizwa. Rasimu kwa sasa inapaswa kupitishwa na wabunge wa Ubelgiji kabla ya Ijumaa usiku wa manane na kisha kupitishwa na Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Msimamo wa pamoja wa Ubelgiji juu ya mkataba wa biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na Canada (Ceta) umesimamishwa, jambo ambalo litapelekea rasimu hiyo kutiliwa saini hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Umbelgiji, Charles Michel amesema Alhamisi hii.

"Makubaliano yamefikiwa", amesema Charles Michel, baada ya mkutano mpya wa mashauriano pamoja na wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali ya Ubelgiji na jamii mbalimbali Alhamisi hii.

Makubaliano hayo kwa sasa yatatumwa kwa Umoja wa Ulaya kabla ya kuwasilishwa kwa mabunge mbalimbali ya Ubelgiji, ambayo yatatoa msmamo wao kuhusu uamuzi huo 'kabla ya Ijumaa usiku wa manane.' Ni "habari njema kwa Ubelgiji katika ngazi ya Ulaya," Charles Michel amepongeza.

"Hatimaye tumefikia makubaliano kati ya Wabelgiji", amesema kwa upande wake Waziri akiwa pia Rais wa jimbo linalozungumza Kifaransa la Wallonia, Paul Magnette, kiongozi wa kambi ya upinzani dhidi ya mkataba wa biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na Canada (Ceta). "Wallonia imefurahisana kuona maombi yetu yamesikilizwa", amekaribisha Paul Magnette.