NIGERIA-UCHUMI

Patience Jonathan alishtaki shirika linalopambana dhidi ya rushwa

Mke wa aliyekua rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, Patience Jonathan.
Mke wa aliyekua rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, Patience Jonathan. REUTERS/Afolabi

Mke wa rais wa zamani wa Nigeria, goodluck Jonathan amefungua mashitaka dhidi ya shirika la kitaifa linalopambana dhidi ya rushwa akilishtumu kuzuia fedha katika baadhi ya akaunti zake za benki.

Matangazo ya kibiashara

Patience Jonathan ameitaka Tume dhidi ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC) kumruhusu kutumia fedha zake na kumlipa dola za Marekani milioni 200, sawa na faranga za CFA bilioni 100 kama fidia kwa ukiukwaji wa haki zake.

Wanawake zaidi ya mia moja wameandamana mbele ya Mahakama Kuu ya mjini Lagos, mji mkuu wa nchi hiyo, dhidi ya kuzuia fedha katika baadhi ya akaunti za benki za Bi Jonathan, hatua iliyochukuliwa na mahakama ya Nigeria.

Tume dhidi ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC) ilizuia baadhi ya akaunti zake za benki tarehe 22 Septemba, kama sehemu ya uchunguzi kwa Patience Jonathan kwa madai ya kujitajirisha kinyume cha sheria, madai ambayo Bi Jonathan anafutilia mbali.

Fedha zilizozuia zinakadiriwa kufikia dola milioni 15, sawa na faranga za CFA bilioni 7.5.

Bi Jonathan atakabiliana na majaji tarehe 7 Desemba, katika sehemu ya uchunguzi ambayo inamkabili.