Wiki ya mwisho yaonekana kuwa ngumu kwa Hillary Clinton
Ikiwa zimesalia siku nane kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, suala la barua pepe la Hillary Clinton, lililozinduliwa na FBI, limeibua hali ya sintofahamu katika kambi ya Wademocrat. Kamati ya maandalizi ya kampeni ya Clinton, ambayo alidhani ina uhakika na ushindi wa mgombea huyo, imejikuta dhaifu. Inabidi kukabiliana na hali hiyo, lakini muda ni mfupi.
Imechapishwa:
Kambi ya Warepublican imeanza kupaza sauti baada ya tukio hilo. Katika kampeni za Donald wamekua wakiimba "gerezani" kwa haraka wakati jina la Clinton lilitangazwa. Katika kampeni ya Clinton, ambayo iliyoendeshwa kwa wakati mmoja, kamati yake imeendelea kumhakikishia mgombea huyo ushindi. Kamati hii inasema itaongeza kasi kwa kuwaeleza wananchi, bila hata hivyo kuwa na imani ya kufaulu kuwaweka sawa wananchi hao na kufanya mabadiliko fulani baada ya kuibuka kwa suala hilo.
Hofu ya ya kujizuia kupiga kura imeendelea kutanda upande wa kambi ya Wademocrat. Miongoni mwa maswali ambayo wengi wamekua wakijiuliza ni pamoja na hili: watafanya nini wapiga kura ambao walipangwa kupiga kura dhidi ya Donald Trump? Matt Lewis, mfuasi wa chama cha Republican anayempinga Trump na mtunzi wa kitabu "Ujinga mwinga kwa lengo la kukosa", Donald Trump hana jambo lolote la kufanya katika wiki hii ya mwisho ya kampeni, "kufunga! Is vizuri kuingilia kati wakati mpinzani wako yuko katika hatua ya kujiangamiza! Trump anapaswa kubaki kimya na kuacha kesi hiyo iendelee, " amesema Bw Lewis.
Hatujui chochote kwa kweli kwa yaliyomo katika ya barua, zilizogunduliwa katika kompyuta ya zamani ya mwenzake Hillary Clinton. Lakini utafiti wa haraka tayari umeonyesha kuvunjika kwa nia ya kupiga kura. Wiki ya mwisho kabla ya uchaguzi inaonekana kutisha kwa mgombea ambaye alianza kuvuma baada ya kuendesha kampeni zake katika maeneo mbalimbali, nchini Marekani.
■ Kuhusu uchunguzi wa barua pepe
Ni lazima kwanza kufafanua kwamba uchunguzi hautaanzishwa kuhusu kompyuta binafsi ya Hillary Clinton, kwa sababu moja tu kwamba uchunguzi umemalizika, lakini faili hii haijafungwa.