DRC-SIASA-UCHUMI

Washirika wa Rais Joseph Kabila matatani

Rais wa DRC, Josephu Kabila, ambaye amesema hakuna kitakachozuia kufanyika kwa uchaguzi
Rais wa DRC, Josephu Kabila, ambaye amesema hakuna kitakachozuia kufanyika kwa uchaguzi DR

Jean-Jacques Lumumba, mmoja wa wajukuu wa mwasisi wa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anawatuhumu washirika kadhaa wa karibu wa Rais Joseph Kabila kwa ubadhirifu wa fedha kupitia benki ya BGFI, ambapo kwa muda mrefu alihudumu kama afisa katika beki hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Shutma hizi zinakuja baada ya mfululizo wa hati zilizowasilishwa kwa gazeti la kila siku la Ubelgiji la Le Soir.

Shutma hizi ni kama bomu dogo kwa wanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.. Katika toleo lake la Oktoba 29, Gazeti la kila sikula Le Soir. limewatuhumumara kadhaa washirika wa karibu wa Rais Joseph Kabila kuwa walifanya mpango wa kifedha wenye mashaka kutoka akaunti zilizofunguliwa katika tawi la benki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya BGFI. Tawi ambalo lilikua likiongozwa na Francis Selemani Mtwale, mshirika wa karibu wa Rais Kabila kwa miaka ambayo aliishi uhamishoni katika ujana wake nchini Tanzania.

"Nilimfikiria babu yangu"

Mtu anayetoa ushahidi huo si mwingine ni afisa wa benki hiyo, Jean-Jacques Lumumba, mmoja w wajukuu wa Patrice Lumumba,mwasisi wa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mtu huyu, mwenye umri wa miaka 30, alijiuzulu kwenye nafasi yake, huku akiondoka na kopi za hati zilizompelekea anapata fursa ya kutoboa ukimya huo.

"Nilichokiona, ilikuwa fedha za watu, aliiambia gazeti la kila siku la Le Soir, kuhusu kazi yake katika benki ya BGFI. Kisha nilimfikiria babu yangu, kwa mapambano yake, kwa kanuni zake. Sitaki kutumia maisha yangu yote katika makosa haya ya dhulma. "

Malipo ya Benki Kuu

Kipengele kingine cha kesi hii ni Albert Yuma, kigogo mwenyekiti wa shirikisho la Biashara la DRC (FEC) na Mwenyekiti wa Bodi ya Gecamines, kampuni ya madini ya serikali. Egal, kampuni ya Yuma inayojihusisha katika biashara ya chakula, ilinufaika mwaka 2013 kwa malipo manne ya jumla ya Dola milioni 43 kwa akaunti iliyofunguliwa kwenye benki ya BGFI. Malipo hayo yalichukuliwa kutoka Benki Kuu ya DRC, taasisi ya serikali inayoongozwa na Deogratias Mutombo Nyembo. Mkopo wa moja kwa moja kwa kampuni ni marufuku. Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Ubelgiji la Le Soir, fedha hizo hazikulipwa.

Aidha, mikopo ya Gecamines kwa benki ya BGFI kwa Dola milioni 30 zilipelekwa kati ya mwezi Oktoba 2015 na Mei 2016, mara mbili kwa faida ya benki. Gharama zilifikia kwa kampuni hiyo ya serikali Dola milioni 2.7. HAta hivyo Albert Yuma anasema ni kosa la benki, lililorekebishwa baadaye

Kwa upande wake Albert Yuma ametaja shutuma kuwa "hazina msingi." "Ni kutokuelewa utendaji wa uchumi kwa kuandika mambo kama hayo, amesema. Bw huyo Lumumba, sijmui. Pengine alilipwa. BGFI itatoa tangazo siku za hivi karibuni na nitajibu binafsi kwa gazeti la kila siku la Le Soir ", Bw Yuma amejitetea.