COTE D'IVOIRE-SIASA

Katiba mpya inayounda Jamhuri ya tatu yapitishwa Cote d'Ivoire

Zoezi la kuhesabu kura wakati wa kura ya maoni ya katiba nchini cote d'Ivoire katika kituo cha kupigia kura mjini Abidjan, Oktoba 30, 2016.
Zoezi la kuhesabu kura wakati wa kura ya maoni ya katiba nchini cote d'Ivoire katika kituo cha kupigia kura mjini Abidjan, Oktoba 30, 2016. REUTERS/Luc Gnago

Hayawi hayawi hatimaye yamekua. Katiba mpya inayounda Jamhuri ya tatu ya Cote d'Ivoire ilipitishwa katika kura ya maoni ya Jumapili Oktoba 30 kwa 93.42% ya kura wakati ambapo upinzani ulikua ulitoa wito wa kususia kura hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Chama tawala na washirika wake pamoja na serikali wameridhishwa na matokeo hayo ya kura, baada ya watu wengi kuwa na mashaka kwamba huenda kiwango cha ushiriki katika kura hiyo ya maoni kikawa kidogo.

Katiba mpya inaazimia kuweka wadhifa wa Makamu wa Rais wa wa Baraza la Seneti, na inaamuru watu wote kwenda shule na inalegeza sheria juu ya uhakiki wa mgombea urais.

Baada ya siku mbili ya kusubiri, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Youssouf Bakayoko alitoa takwimu za kwanza katika ngazi ya kitaifa "kiwango cha ushiriki kilifikia 42.42%. Kura ya "Ndiyo", ilipitishwa na sauti milioni 2.48, sawa na 93.42% ya kura. Kura ya "Hapana" ilipata sauti 174,714 sawa na 6.58% ya kura. "

Pamoja na matokeo haya ya 93% kwa kura ya "ndiyo" na kiwango cha ushiriki kuwa juu zaidi kwa kura ya maoni ya Jumapili iliyopita, muungano wa vyama vinavyounga mkono serikali wa RHDP una imani ya kuundwa kwa Jamhuri ya tatu yacote d;Ivoire.Hatua inayofuta ni kusahihishwa kwa matokeo hayo na Baraza la Katiba.

Lakini hata kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kura ya maoni katika ngazi ya kitaifa, upinzani ulishutumu, ukisema kwamba kiwangocha ushiriki kilikua kati ya 3% na 7%. Baadhi ya wapinzani wamebaini kwamba "kulifanyika ujajna fulani kwa kubadilisha matokeo ya kura ya maoni na kutoheshimu utaratibu wamatangazo ya matokeo. "