MAREKANI-SIASA-UCHAGUZI

Wagombea urais Marekani waendelea kutupiana vijembe

Donald Trump na Hillary Clinton wameendelea na mfululizo wa kampeni katika kinyang'anyiro cha kuwania urais Marekani.
Donald Trump na Hillary Clinton wameendelea na mfululizo wa kampeni katika kinyang'anyiro cha kuwania urais Marekani. REUTERS/Carlos Barria

Wagombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican wameshambuliana vikali wakati huu kampeni zikiwa katika dakika za lala salama kuelekea Uchaguzi Mkuu wiki ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Bi.Clinton akizungumza katika jimbo la Florida, amemshtumu Trump kwa kuwabagua na kuwadhalalisha wanawake, na kusisitiza kuwa hafai kuwa rais wa Marekani.

“Tuna mtu anayewania urais ambaye anadhalalisha watu lakini pia ni mtu pekee ambaye kwa muda wa miaka 40 hajalipa kodi.Halafu anapata nguvu ya kulishuytumujeshi letui na kuwatusi watu wengine, na hajalipa chochote hasa kwa wanajeshi wetu. Kwa hivyo ukimwona mtu anasema anampigia kura Trump, msaidie kwa kumshauri.”

Trump naye amemshtumu Bi.Clintion kama mtu fisadi ambaye ataharibu uongozi wa Marekani, na kuwataka wapaiga kura kufanya uamuzi makini wiki ijayo.

“Uchaguzi unakuja, sijui kama mtakuwa na nafasi nyingine tena. Ikiwa Clinton atachaguliwa, itakuwa hatari sana hasa kwa katiba ya nchi yetu.Kutokana na kashfa inayomkubwa huenda akaendelea kuchunguzwa kwa miaka mingi ijayo na suala hili kuishiwa yeye kufunguliwa mashtaka makubwa.”

Wagombea hao wawili wanatumia mikutano hii ya mwisho, kuwahamasisha wapiga ambao tayari wameshapiga kura kubadilisha kura zao na kuwapigia kura kuelekea tarehe 8, siku ya mwisho ya kupiga.

Hillary Clinton amekuwa akiendelea kukabiliana na sakata la kufuta barua pepe alipokuwa Waziri wa Mambo ya nje, suala ambalo linachunguzwa na shirika la FBI, hatua ambao chama cha Democratic kimehstumu.