AFRIKA KUSINI-RUSHWA

Wito wa kujiuzulu kwa Rais Zuma waendelea kutolewa nchini Afrika Kusini

Mjini Pretoria, wakati wa mkutano wa hadhara kwa kumuomba Jacob Zuma kujiuzulu, Novemba 2, 2016.
Mjini Pretoria, wakati wa mkutano wa hadhara kwa kumuomba Jacob Zuma kujiuzulu, Novemba 2, 2016. REUTERS/Siphiwe Sibeko TPX IMAGES OF THE DAY

Tangu Jumatano hii, Novemba 2, wito wa kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma umeendelea kuongezeka nchini Afrika Kusini. Upinzani wa kisiasa, vyama vya kiraia, na watu binafsi, kwa jumla raia wa Afrika Kusini wamesema kughadhabishwa na mafunuo ya ripoti juu ya uhusiano kati ya rais wao na familia ya watu tajiri ya Gupta kutoka India.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya mahakama kuamuru kuchapiswa kwa ripoti inayomhusisha Rais Jacob Zuma na Mawaziri wake vigogo kwa madai ya rushwa, upinzani na mashirika ya kiraia wameendelea kutoa wito wa kujiuzulu kwa Rais Zuma. Mita mia moja kutoka jengo la mahakama, Julius Malema, mmoja kati ya viongozi waupinzani, aliwatolea wito wafuasi wake kuandamana hadi kwenye makao makuu ya serikali. "Zuma yuko mfukoni mwa familia ya Gupta. Na ni jambo la kawaida sisi kuomba aondoka mamlakani. Anapaswa kuachia ngazi kwa sababu hana tena hadi ya kuendelea kushikilia madaraka."

Kwa upande wake Zwelinzima Vavi, mkuu wa zamani wa Cosatu, muungano wa vyama vya wafanyakazi unaoshirikiana na serikali, amesema "siyo mkuu wa nchi pekee ambaye anapaswa kuondoka, lakini pia wale wote ambao walimuunga mkono. Wale wote ambao walikua wakimpongeza Bungeni, serikalini, watu wote hawa wanapaswa kuondoka. Wale wote ambao waliomzomea msuluhishi wa Jamhuri kwa kumlinda mkuu wa nchi. "

Kuelekea kupiga kura ya kutokua na imani

vyama kahaa vya upinzani tayari vimetangaza kuanzisha utaratibu wa kupiga kura ya kutoa kuwa na imani dhidi ya rais Jacob Zuma wiki ijayo. "Huu ni ushindi kwa demokrasia na mamlaka ya kikatiba, amesema Mmusi Maimane, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance. "Tulipambana mahakamani kwa ajili ya kuchapishwa kwa ripoti hii" ameongeza Bw. Maimane.