MAREKANI-SIASA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa Marekani 2016: Trump na Clinton watupiana vijembe

Donald Trump na Hillary Clinton washambuliana katika kampeni zao.
Donald Trump na Hillary Clinton washambuliana katika kampeni zao. REUTERS

Wagombea urais nchini Marekani Donald Trump wa chama cha Republican na Hillary Clinton wa chama cha Democratic wameshambuliana kwa mara nyingine ni nani anaweza kuwa rais bora.

Matangazo ya kibiashara

Bi. Clinton kwa mara nyingine amesema Trump hana sifa za kuwa rais lakini pia amedhihirisha wazi kuwa amewadhalilisha wanawake nchini Marekani.

Trump naye amesema ikiwa Clinton atachaguliwa, atakuwa rais mshukiwa wa kashfa mbalimbali na kusisitiza kuwa hana sifa za kuwa rais.

Kwa mara ya kwanza mke wa Trump, Melania Trump ameonekana akimfanyia kampeni mume wake na kumwelezea kama mtu sahihi kuongoza Marekani.

Rais Barrack Obama kwa upande wake, ameendelea kuwashinikiza wafuasi wa chama cha Democratic hasa vijana kujitokeza kwa wingi na kumpigia kura Bi.Clinton siku ya Jumanne Novemba 8, 2016.