Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia ushindi wa mgombea wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, ambaye amemuangusha vibaya mgombea wa Democrat, Hillary Clinton, ambaye amekubali kushindwa.Ushindi wa Donald Trump unaashiria nini kwa uchumi na usalama wa dunia? ungana na mtayarishaji wa makala haya kufahamu mengi.
Vipindi vingine
-
Gurudumu la Uchumi Umuhimu wa bara la Afrika kuwa na mfumo wa pamoja wa kufanya malipo kidijiti Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, malipo ya kidijiti au ya kimtandao yanachangia pakubwa katika kujenga msingi imara wa kufikia maendeleo endelevu, kwanini? Ni kwasababu malipo haya yanapokuwa rahisi, salama, ya wazi na binafsi, yatawezesha ukuaji wa fursa kama nishati, maji na mikopo.Katika kipindi hiki utamsikia, Lucy Nshuti Mbabazi, kutoka taasisi ya umoja wa Mataifa ya muungano wa Better than Cash, Lacina Kone, mkurugenzi wa Smartafrica pamoja na Kwizela Aristide Basebya, mtafiti wa Teknolojia za Mawasiliano ya Umma na Matumizi yake serikalini, akiwa Beijing, China.17/05/2023 10:00
-
Gurudumu la Uchumi SmartAfrica: Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo - Sehemu ya Pili Msikilizaji mataifa mengi ya Afrika, sasa hivi yanafanya juhudi kuhakikisha raia wake wanaunganishwa na huduma ya internet, kama moja ya harakati za kuchochea maendeleo kupitia teknolojia.Lakini kwa wananchi kuunganishwa na huduma hiyo ni jambo moja, changamoto iliyoko sasa hivi kwa nchi nyingi za Afrika ni kukosekana kwa miundombinu sahihi kuwezesha hilo.10/05/2023 10:01
-
Gurudumu la Uchumi Smart Afrika:Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo - Sehemu ya Kwanza Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo, ni moja ya ajenda iliyojadiliwa kwa kina katika mkutano wa juma lililopita nchini Zimbabwe, kuhusu namna bara la Afrika linaweza kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano, TEHAMA, kubadili uchumi wake na kurahisisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi wa bara hilo kama vile afya na kilimo.10/05/2023 10:02
-
Gurudumu la Uchumi Miaka 2 madarakani ya Rais wa Tanzania Wataalamu wa uchumi na diplomasia wanasema, katika muda mchache aliokuwa madarakani, ameonesha dhamira ya kutekeleza mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini Tanzania, mbali na uchumi, ameshughulikia masuala ya kisiasa na kusaka maridhiano ya kitaifa, wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunaangazia miaka miwili madarakani ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.24/03/2023 10:04
-
Gurudumu la Uchumi Siku ya wanawake duniani na ushiriki katika ngazi za maamuzi Msikilizaji hebu fikiria kuwa na dunia yenye usawa. Dunia huru ya bila upendeleo na ubaguzi. Dunia jumuishi, yenye kutoa haki na shirikishi. Dunia ambayo licha ya tofauti zetu lakini bado tunaheshimiana na kufurahia. Na leo hii wataalamu wanatuambia tunaweza kusimama pamoja kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa wote bila ubaguzi wa wanawake.24/03/2023 10:02