MAREKANI-SIASA

Michelle Obama aombwa kuwania mwaka 2020

Michelle Obama, mkewe Rais Barack Obama, Washington Mei 8, 2014.
Michelle Obama, mkewe Rais Barack Obama, Washington Mei 8, 2014. REUTERS/Yuri Gripas

Mamia ya raia wa Marekani tayari wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais wa Jumanne wiki hii kumhumiza Michelle awanie katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

Watu wengi nchini Marekani wameanza kufikiria uchaguzi wa mwezi Novemba 2020 kuhusu nani ambaye anafaa au ana sifa nzuri ya kuwania uchaguzi wa mwaka 2020.

Baadhi wameandika "Mazingira ni mazuri kwa Michelle Obama kushinda uchaguzi 2020".

Wengine wameandika "Michelle Obama tunakuomba tafadhali uweze kuwania katika uchaguzi wa mwaka 2020, tafadhali tunakuomba".

Kwa mujibu wa utafiti wa Gallup, Michelle Obama anapendwa asilimia 64 na Wamarekani, kiwango kilicho juu ya Donald Trump, Hillary Clinton na hata mumewe.

Licha ya mapendekezo hayo, Michelle Obama mapema mwezi Machi alisema hana nia ya kuwania urais.

Mke wa Rais Obama, Michelle Obama, ambaye kando na kuwa mwanamke kama Bi Clinton, ameonyesha kuwa na sifa nzuri.