MAREKANI-CUBA-TRUMP

Uchaguzi wa Donald Trump, pigo kwa raia wengi wa Cuba

Watetezi wengi wa jitihada za kufufua uhusiano wa Marekani na Cuba wana hofu kuwa jitihada hizo huenda zikasimama kufuatia kuchaguliwa kwa Donald Trump.
Watetezi wengi wa jitihada za kufufua uhusiano wa Marekani na Cuba wana hofu kuwa jitihada hizo huenda zikasimama kufuatia kuchaguliwa kwa Donald Trump. REUTERS/Enrique De La Osa

Ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais nchini Marekani umepokelewa na wasiwasi na Wacuba wengi. Kwa uhakika, wanahofia kuona juhudi za kufufua uhusiano kati ya nchi yao na Marekani zinaweza kuambulia patupu.

Matangazo ya kibiashara

Mfanyabiashara huyo tajiri wa Marekani aliwahi kusikika akisema kuwa atarejelea baadhi ya mambo yaliyoafikiwa na Barack Obama kwa utawala wa kikomunisti katika maamuzi ya kuzuia mali za Cuba mwishoni mwa mwaka 2014.

Kufuatia hali hiyo, Rais wa Cuba Raul Castro, mtetezi pamoja na mwenzake wa Marekani Barack Obama, wa kufufua uhusianokati ya Washington na Havana, amempongeza Donald Trump, mshindi wa uchaguzi wa urais wa Marekani Jumatano, Novemba 9.

Serikali ya Cuba imetangaza katika gazeti la serikali kufanyika katika siku za usoni kwa mazoezi mapya muhimu ya kijeshi kwa lengo la kukabiliana na uwezekano wa uvamizi.

Kama harakati hizi zitawekwa katika vitendo, huenda hali ikawa mbaya zaidi katika siku za usoni kuhusu uhusiano kati ya maadui wawili wa zamani wa vita baridi wakati Trump atachukua hatamu ya uongozi wa nchi mwezi Januari mwakani.

Nchini Cuba, wakazi wengi tayari wameonyesha wasiwasi wao juu ya uchaguzi wa Donald Trump. Bw, Trump alitangaza miezi ya hivi karibuni keamba anapinga uamuzi wa kufutwa vikwazo vya kifedha na kibiashara vilivyowekewa Cuba tangu 1962.

Wapinzani wa Castro wamuunga mkono Donald Trump

Uchaguzi wa Donald Trump umesababisha raia wengi wa Cuba kukata tamaa. Donald Trump alipozuru Florida tarehe 21 Oktoba, wakati alikuwa bado mgombea, alikutana na wapinzani wa utawala wa kikomunisti na alisema anawaunga mkono kwa harakati zao.