DRC-SIASA

Joseph Kabila kumteua Waziri Mkuu

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA

Jumatatu hii, Novemba 14 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, anatazamiwa kumteua mrithi wa Augustin Matata Ponyo kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyotokana na mazungumzo, Waziri Mkuu atateuliwa kutoka miongoni mwa wapinzani, ambapo sehemu mona ya upinzani ilishiriki katika mazungumzo na serikali pamoja na vyam avinavyoiunga mkono. Mpaka sasa hajajulikana mtu ambaye atashikilia nafasi hii muhimu nchini humo.

Majina kadhaa ya wanasiasa wa upinzani yamekua yakizungumzwa na wakazi mbalimbali mjini Kinshasa kuwa huenda mmoja wao akateuliwa kwenye wadhifa huo.

Anayepewa nafasi kubwa kwa kushikilia wadhifa wa Waziri Mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni Vital Kamerhe, ambaye ni mmoja miongoni mwa wapinzani aliyefanya kiliyochini ya uwezo wake ili kufanyike mazungumzo kati ya serikali na sehemu moja ya upinzani. Alionekana akiongoza upinzani uliyoshiriki mazungumzo hayo na serikali. Wengi mjini Kinshasa wanaamini kuwa wadhifa huo huenda ukashikiliwa na kiongozi wa chama cha UNC kwa kazi alioifanya katika mazungumzo hayo.

Makamu wa zamani wa rais Azarias Ruberwa pia ameombwa kukubali kushikilia wadhifa huo hadi mwezi Aprili 2018.

Pamoja na wawili kutoka mkoa wa Kivu ya Kusini, pia jina la Seneta Florentin Mokonda Bonza, mtu wa karibu sana na Léon Kengo wa Dondo, rais wa Baraza la Seneti. Waziri wa zamani na mkuu wa wafanyakazi kwenye Ofisi ya rais Mobutu Sese Seko, ambaye ni kutoka mkoa wa zamani wa Mashariki ana uzoefu na anaonekana kuwa anaweza kuteuliwa kwenye wadhifa huo kutokana na umaarifu wake.

Eneo la Magharibi halitaki kubaki nyuma kwenye mbio hizo. Leon Kengo wa Dondo mwenyewe ananyooshewa kidole na wachambuzi kwa sababu ya uzoefu wake na umri. Mwanasheria, balozi na mara kadhaa Waziri Mkuu chini ya utawala wa Mobutu Sese Seko, Leon Kengo wa Dondo, hata hivyo, anapendelea kuteuliwa kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu Waziri wa sasa wa Bajeti, Michel Bongongo, kutoka mkoa wa zamani wa Equateur kama Bw Kengo wa Dondo.

Kwenye mitandao ya kijamii, pia jina la Felix Tshilombo Tshisekedi kwa niaba muungano wa Rassemblement limekua likitajwa. Lakini muungano huu wa upinzani unaosimamiwa na Etienne Tshisekedi pamoja na Moise Katumbi bado haujamaliza mazungumzo katika ngazi ya Baraza Kuu la Maaskofu nchini DRC (Cenco). Jumatatu hii, muungano wa Rassemblement na kundi la mazungumzo watakutana pamoja, katika kamati ndogo, pamoja na Maaskofu kwa mazungumzo ya moja kwa moja.