GUINEA-SIASA

Rais Jose Mario Vaz atangaza kuifuta serikali

Rais wa Guinea-Bissau Jose Mario Vaz ametangaza Jumatatu kuifuta serikali inayoongozwa tangu Juni na Waziri Mkuu Baciro Dja. Timu mpya itaundwa kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa mjini Conakry mwezi mmoja uliopita ili kuondokana katika mgogoro wa kisiasa unaoendelea kuikumba nchi hiyo. 

Rais wa Guinea-Bissau, Jose Mario Vaz, Juni 11, 2014.
Rais wa Guinea-Bissau, Jose Mario Vaz, Juni 11, 2014. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Rais Jose Mario Vaz alieleza Jumatatu Novemba 14 kuwa "makubaliano ya mjini Conakry hayasemi kupitishwa kwa waziri mkuu kwa kauli moja, lakini kwa makubaliano, na makubaliano hayakuweza kufikiwa." José Mario Vaz alisema kuwa yuko tayari "kuifuta serikali" iliyopo na "kuteua waziri mkuu mpya ambaye atakuwa na jukumu la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa minajili ya kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro mgogoro wa kisiasa unaoikumba."

Hakuna muda uliyotolewa kwa uteuzi wa waziri mkuu mpya, chanzo kutoka Ofisi ya rais kimebaini kwamba waziri huyo atateuliwa "hivi karibuni." Tangazo hili linafuatia ziara, mapema mwezi Novemba, ya ujumbe wa tume ya usuluhishi katika ukanda huo ulioongozwana Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kwa kuzishinikiza pande husika katika mgogoro huo kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa tarehe 14 Oktoba mjini Conakry chini ya mwamvuli wa Rais wa Guinea Alpha Conde.

Mvutano na PAIGC

Uamuzi huu haujamaliza mgogoro wa kisiasa unaoathiri nchi hii tangu Rais Vaz Waziri achukuwe uamuzi, mwezi Agosrti 2015, wa kumfuta kazi Waziri Mkuu Domingos Simões Pereira, mkuu wa Chama cha PAIGC, chama cha Rais Vaz.

Kwa hakika, chama cha PAIGC, aambacho kilikua kikipinga uteuzi wa Baciro Dja, mwezi Juni, hakitambui uamuzi wa rais wa kumfukuza au kumteua waziri mkuu. Kama makubaliano ya mjini Conakry yanatoa kanuni ya 'mchakato wa makubaliano' kwa kumchagua kiongozi 'ambaye rais ana imani naye,' ni, kulingana na Katiba, kwa chama chenye wabunge wengi kumchagua Waziri Mkuu.

Lakini chama cha PAIGC kilipoteza idadi kubwa ya viti vya Wabunge kwa kupata 57 kati ya 102 kufuatia kuiojiondoa kwa chama hicho kwa Wabinge 15.