Gurudumu la Uchumi

Kizungumkuti kuhusu ufadhili wa fedha kwa bara la Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Sauti 09:41
Wakuu wa nchi za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakati waliposhiriki mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Marrakech, Morocco. November 16, 2016.
Wakuu wa nchi za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakati waliposhiriki mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Marrakech, Morocco. November 16, 2016. REUTERS/Youssef Boudlal

Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili imeangazia yanayojiri kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, CP22, unaofanyika mjini Marrakech, Morocco, ambako mataifa yanakutaja kujadili na kuanza kutekeleza mkataba wa Paris uliotiwa saini mwaka uliopita.Nchi zilizoendelea ziliahidi kulichangia bara la Afrika kiasi cha fedha ili kuziwezesha kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini bado mvutano ni mkubwa kuhusu masharti na namna fedha hizo zinavyotolewa, huku wataalamu wakionya uchumi wa dunia kuteteraka ikiwa nchi hazitakubaliana sasa.