MAREKANI-UCHAGUZI 2016

Maneno ya kibaguzi yamlenga Michelle Obama, Meya ajiuzulu

Meya wa mji wa Virginia Masharki, nchini Marekani, alijiuzulu Jumanne wiki hii Novemba 15 baada ya kusababisha hali ya sintofahamu kwa kukaribisha maoni ya kibaguzi kuhusu Michelle Obama. Kiongozi huyo aliyetoa hotuba isiyokubalika ameadhibiwa.

Michelle Obama Oktoba 27, 2016 katika mkutano wa hadhara wa chama cha Democratic katika mji wa Winston-Salem, North Carolina.
Michelle Obama Oktoba 27, 2016 katika mkutano wa hadhara wa chama cha Democratic katika mji wa Winston-Salem, North Carolina. Jewel SAMAD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa mji wa Clay katika jimbo la Virginia Mashariki wamepigwa na bumbuwazi. Meya wa mji wa Clay amepakwa amenyooshewa kidole na waandishi wa habari au simu zake alizokua akiongea akiwa na hasira.

Chanzo cha kashfa hii, Pamela Taylor Ramsey, mkurugenzi wa shirika la misaada, baada tu ya kuchaguliwa Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook: "Hatimaye ninajisikia nina furaha kuona mwanamke mzuri katika Ikulu ya White House, kwenye nafasi ya heshima kama hii. Nimechoshwa na kuona tumbili wakiwa wamesimama mbele za watu." Maneno haya yalimfurahisha Meya wa mji wa Clay, ambaye alijibu kwenye Facebook, "Umenifurahisha kwa siku ya leo." Tangu wakati huo maneno haya ya Clay yalifutwa.

Wanawake hawa wawili wamejiuzulu, na Halmashauri ya jiji imeomba radhi. Halmashauri ya jiji imewataka waandishi wa habari kutembeleamji huo wenye wakazi 500 katikati mwa Marekani uliyompigia kura Donald Trump. "Sisi ni watu wenye heshima, tafadhali, walamsithukumu kwa kesi hii." Watu zaidi ya 200,000 walitia saini kwa muda wa saa 24 kwenye waraka unaopinga kauli hizo za ubaguzi wa rangi.