CAR-EU

CAR yakubaliwa kupewa Dola bilioni 2.2 kwa kuendeleza miradi yake

Wafadhili wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) waliokutana Alhamisi wiki hii jijini Brussels nchini Ubelgiji, wameahidi kutoa msaada wa hadi dola bilioni 2.2 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kama kujibu ombi la rais Faustin-Archange Touadéra wa nchi hiyo ili kuijenga upya nchi.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje Federica Mogherini mjini Brussels Novemba 17, 2016
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje Federica Mogherini mjini Brussels Novemba 17, 2016 EMMANUEL DUNAND / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jamhuri ya Afrika ya kati iliingia kwenye vita kati ya waasi wa Kikiristo na wale wa Kiislamu mwaka 2013 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Kiongozi wa nchi hiyo amewaambia wafadhili na marafiki wa nchi hiyo wanaokutana jijini Brussels nchini Ubelgiji kuwa nchi yake inapitia kipindi kigumu na inahitaji Dola Bilioni 3.0 kwa muda miaka mitano ijayo ili kurejea katika hali ya kawaida.

 

DDR, mageuzi ya vikosi vya usalama, kuboresha vyombo vya sheria na maridhiano vinapaswa kupewa kipaumbele katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Touadera. Miongoni mwa wafadhili wakuu: Benki ya Dunia imetoa zaidi ya Dola milioni 500 na Tume ya Ulaya imeahidi milioni 450. "Mimi nimeona wasiwasi wa baadhi ya wafadhili kuhusu uwezo wetu katika masuala ya rasilimali," amesema Rais Touadéra ambaye ametoa ameahidi wafadhili wake kuwa atatekeleza haraka mpango huo mageuzi. katika nyanja mbalimbali.