UFARANSA-SIASA

Kura za mchujo Ufaransa: mjadala wa mwisho wafanyika katika hali ya sintofahamu

Jean-Fraçois Copé, Nicolas Sarkozy, Alain Juppé, Nathalie Kosciusko-Morizet, Jean-Frédéric Poisson, François Fillon na Bruno Le Maire Alhamisi Novemba 17 katika ufunguzi wa mjadala wa mwisho.
Jean-Fraçois Copé, Nicolas Sarkozy, Alain Juppé, Nathalie Kosciusko-Morizet, Jean-Frédéric Poisson, François Fillon na Bruno Le Maire Alhamisi Novemba 17 katika ufunguzi wa mjadala wa mwisho. REUTERS/Christphe Archambault/Pool

Mjadala wa mwisho wa moja kwa moja kupitia runinga kwa ajili ya uchaguzi wa awali umefanyika Alhamisi hii Novemba 16 ambapo wagombea wameshindwa kutoa ahadi zinazo washawishi wapiga kura ikiwa ni siku mbili kabla ya uchaguzi huo wa Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Mjadala uligubikwa na hali ya sintofahamu, wakati mwingine kurushiana vijembe na lawama, majibu yenye kejeli kutoka kwa Nicolas Sarkozy kuhusu kesi iliyokua ikimkabili, huku watu watatu wanaopewa nafasi kubwa wakiejepusha kukabiliana

Kama katika mjadala wa kwanza, maneneo ya kejeli na lawama viliibua hali ya sintofahamu katika dakika za kwanza za kipindi hiki kiliyorushwa moja kwa moja kwenye runinga ya Franc 2 na Europe 1. Akiulizwa kuhusu tuhuma dhidi yake kuhusu maswala ya kisheria yanayomkabili kwa sasa hususan swala la kupokea pesa kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya marehemu Muamar Gadaffi, Nicolas Sarkozy ameonekana kupuuzia tuhuma hizo, huku akimshambuliwa mwandishi wa habari Daudi Pujadas aliyeuliza swali hilo. "Aibu gani! Hauna aibu ya kumpa nguvu mtu ambaye alifungwa, ambaye alihukumiwa kwa kosa la kumkashifu rais na isitoshe mtu ambaye ni mwongo? "Alijibu rais wa zamani Nicolas Sarkozy, huku akitaka kesi hiyo isirejelei ten akatika kipindi hicho.

Dalili nyingine ya hasira: Bruno Le Maire, ambaye alitafautiana na François Fillon katika uchaguzi, alijibu kwa kejeli swali la mwandishi wa habari Jean-Pierre Elkabbach kuhusu kampeni zake: "Mimi ni mgombea katika kura za mchujo, ninaomba tu heshima kutoka kwako. "

Wagombea Jean-François Cope, Nicolas Sarkozy, Alain Juppe, Nathalie Kosciusko-Morizet, Jean-Frédéric Poisson, François Fillon na Bruno Le Maire wanawania nafasi ya uteuzi wa kukiwakilisha chama cha mrengo wa kulia cha UMP kwenye uchaguzi wa rais hapo mwakani.

Takwimu zinaonyesha kuwa Alain Jupe anakuja mbele na kumshinda pointi moja Nicolas Sarkozy huku waziri mkuu wa zamani Francois Fillon akichukuwa nafasi ya tatu.