CHAD-SIASA

Wapinzani wakamatwa wakati wa maandamano nchini Chad

Sokoni mjini Ndjamena, nchini Chad.
Sokoni mjini Ndjamena, nchini Chad. ISSOUF SANOGO / EUROPEAN-COMMISSION / AFP

Nchini Chad, wapinzani wengi walikamatwa Alhamisi Novemba 17 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ndjamena, walipokua wakiandamana wakati ambapo serikali ya Rais Idriss Deby Itno imepiga marufuku mkutano wa hadhara wa chama cha upinzani na kukataliwa pendekezo lake bungeni juu ya mgogoro wa kijamii.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani uliwataka wafuasi wake kukusanyika katika uwanja wa mpira wa Abena katika kata ya 7 ya mji mkuu wa Chad ili kuonyesha hasira kuhusu mgogoro wa kijamii unaoendelea nchini humo.

Lakini mapema Alhamisi, polisi walizingira uwanja huo wa mpira na kuzuia wafuasi kuingia, wafuasi ambao walilazimika kurudi nyuma na kuelekea kwenye makao makuu ya chama cha UNDR, chama cha kiongozi mkuu wa upinzani.

Baada ya muda, kiongozi wa chama cha upinzani cha RDR, alitoa wito kupinga marufuku hayo. "Msikubali kutii amri ya hiyo ambayo ni kinyume cha sheria na katiba. Sisi tutapinga, tutapigana kwa ajili ya nchi yetu! "