CHAD-IASA-UCHUMI

Chad yaendelea kukabiliwa na migogoro mbalimbali

Rais wa Chad Idriss Deby, Januari 31, 2016.
Rais wa Chad Idriss Deby, Januari 31, 2016. REUTERS/Tiksa Negeri

Chad, ambayo ni mshirika mkuu wa nchi za Magharibi katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa kijihadi barani Afrika, inaendelea kukumbwa na mgogoro wa kisiasa ambao unaukabili utawala wa kiimla wa Idriss Deby wakati ambapo upinzani umewataka wananchi kususia kazi siku ya Jumanne Novemba 22.

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Chad imepata pigo kubwa kwa kuingilia kijeshi dhidi ya kundi la wanajihadi la Boko Haram, kuanguka kwa mapato ya mafuta, upungufu na hatua kali, mgomo wa wafanyakazi kwa miezi kadhaa sasa, mdororo wa uchumi na kadhalika. "Chad kwa sasa imeanguka. Tunaogopa kutokea kwa hali ya hatari, " msemaji wa muungano wa vyama vya kiraia, Maoundoe Decladore, ameliambia shirika la habari la AFP, huku akisema "mambo yatabadilika".

Mgogoro na hasira ya wananchi vimeliweka mashakani soko kuu la N'Djamena. "Natumia siku nzima kwa faranga 1,000 tu (sawa na Euro 1,50). Hakuna fedha. Watu hawaji, " Fatima Zara, muuza mbogamboga, mwenye umri wa miaka arobaini, amelalamika.

Walimu wamekuwa katika mgomo tangu mwezi Septemba wakiudai malipo ya malimbikizo ya mishahara. "Fedha zote za mafuta zilipitishwa mlango wa nyuma na watu wa utawala" amejilaumu Michel Issa, mwalimu wa chuo, akijiunga na vyama vya kiraia na upinzani, kwa kuinyooshea kidole cha lawama familia na kabila la rais Idriss Deby kwa "utawala mbaya".

Matokeo: hakuna mwaka wa shule katika shule mbalimbali nchini Chad, vyuo na vyuo vikuu, ambavyo kunahatari vifunge mwaka mzima. sekta nyingine zinazokabiliwa na hali ngumu ni pamoja na afya, na kusababisha wagonjwa kutafuta matibabu nchini Cameroon, pamoja na sekta ya sheria. Rais Deby mwenyewe aliwapokea siku ya Ijumaa mahakimu akiwataka wasitishe mgomo wao.

Hali ni mbaya nje ya mji mkuu wa nchi hii maskini, yenye wakazi milioni 10, ambapo zaidi ya mtoto mmoja aliye na umri ulio chini ya miaka mitano kwa watoto watatu akabiliwa na matatizo ya ukuaji.