MOROCCO-SIASA

Mzozo wa kisiasa kutokea Morocco

Waziri Mkuu wa Morocco Abdelilah Benkirane akabiliwa na hali ngimu ya kuunda serikali ya muungano.
Waziri Mkuu wa Morocco Abdelilah Benkirane akabiliwa na hali ngimu ya kuunda serikali ya muungano. © Fadel Senna/AFP

Wiki sita baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa wabunge nchini Morocco, Waziri Mkuu Abdelilah Benkirane bado hajaweza kuunda serikali ya muungano, hali ambayo inaweza kupelekea nchi hii kutumbukia katika mgogoro wa kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya ushindi wa chama chake cha PJD, Bw. Benkirane aliteuliwa kwa mara nyingine na Mfalme nchi hiyo kuwa waziri Mkuu wa serikali ya muungano anayoongoza kwa miaka mitano.

Tangu wakti wa uteuzi wak, amekua akifanya mazungumzo na vyama vinavyowakilishwa bungeni, isipokuwa wapinzani wake mashuhuri wa chama cha PAM, kiliyochukua nafasi yapili katika uchaguzi huo.

Hata hivyo Abdelilah Benkirane bado haijaweza kukusanya idadi ya wabunge 198 ambao watamhakikishia kura ya imani bungeni, ambapo chama chake kilishinda kwa kupata viti 125 bungeni.