DRC-SIASA

Rassembement: Joseph Kabila afikia mwisho wa muhula wake

Joseph Kabila, rais DRC, mbele ya bunge la DRC, Novemba 15, 2016 mjini Kinshasa.
Joseph Kabila, rais DRC, mbele ya bunge la DRC, Novemba 15, 2016 mjini Kinshasa. © Junior D.Kannah/AFP

Muungano wa vyama vya upinzani wa Rassemblement, ulitoa wito Jumamosi kwa wafuasii wake kuandamana nchini kote ili kumuonya rais Joseph Kabila kuwa muhula wake umefikia tamati. Lakini vikosi vya usalama vilitawanya kundi la wapinzani katika miji mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Lubumbashi, mji wa pili kwa ukubwa ambapo maandamano na mikutano ya hadhari imepigwa marufuku kwa mwaka mmoja sasa, waandamanaji waliojaribu kujiunga na muungano wa vyama vya upinzani wa Rassemblement, walikamatwa na askari.

Kwa ujumla, shughuli zilizorota kwa sababu ya uwepo mkubwa wa polisi na wanajeshi wa jeshi laJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Nyumba za wapinzani zashambuliwa

Polisi ilizuiwa Antoine Gabriel Kyungu wa Kumwanza, kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani wa Rassemblement katika mkoa wa zamani wa Katanga, kuwasili katika eneo lililokuwa lilipangwa kufanyiaka mkutano. Na makazi binafsi ya Charles na Christian Mwando, makada wawili wa kambi muungano huo wa upinzani, walishambuliwa ghafla mawe katika mji wa Lubumbashi na kundi la vijana wasiojulikana.

Christian Mwando, waziri wa zamani wa fedha kimkoa, alishambuliwa, huku kukiwepo na magari ya polisi

Kabla ya kutawanywa, "watu hawa walipewa muda wa kuharibu nyumba yangu, magari na madirisha vilivunjwa. Baada tukio hilo, walikwenda kwenye makazi ya baba yangu, Charles Mwando, mwenyekiti wa kundi linalomuunga mkono Moise Katumbi. Waliingia ndani ya nyumba na kuharibu kila kitu. Piawaliharibu magari na kuahidi kuwa watarudi. Wakati huo huo, majirani zangu walimkamata askari polisi ambaye alikuwa katika kundi la washambuliaji na mtu anayedai kuwa muuzaji wa mafuta, " alieleza Mwando Christian kwenye radio Okapi.