BURUNDI-SIASA

Kanisa katoliki latoa wito kwa mazungumzo nchini Burundi

Kanisa Katoliki nchini Burundi limetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo na upinzani ili kuwezesha kurudi kwa maelfu ya wakimbizi wa Burundi waishio uhamishoni.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akosolewa kwa kutaka kuzua suala la ukabila kwa kutenga watu kutoka jamii fulani katika mashirika ya umma na vikosi vya ulinzi na usalama.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akosolewa kwa kutaka kuzua suala la ukabila kwa kutenga watu kutoka jamii fulani katika mashirika ya umma na vikosi vya ulinzi na usalama. ????
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Burundi, Gervais Banshimiyubusa amesema kuwa mazungumzo yanaihitajika ili kumaliza mgogoro huo.

"Wakati wanasiasa wataendelea kuwachukulia wale ambao si kutoka kambi yao kama maadui, mazungumzo hayatawezekana," Askofu Banshimiyubusa amesema.

"Watu hawakai na maadui zao, badala yake wanawakimbia," ameongeza.

Askari wa Burundi wakipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, baada ya shambulio la guruneti, Februari 3, 2016.
Askari wa Burundi wakipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, baada ya shambulio la guruneti, Februari 3, 2016. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama

Spika wa Bunge ajitetea

Hali ya kisiasa imeimarika na inatosha tu kuwajulisha wakimbizi ili waweze kurudi nyumbani, Spika wa Bunge la Burundi Pascal Nyabenda aliwaambia Maaskofu Jumapili Novemva 20 wakati wa sherehe za kidini.

Visa vya ukandamizaji vinavyoendeshwa na utawala tangu Rais Pierre Nkurunziza kuchukua uamuzi, mwezi Aprili mwaka 2015, wa kuwania muhula mwingine, vimeendelea kushuhudiwa nchini humo.

Maiti zikiokotwa katika mitaa ya Bujumbura asubuhi ya Desemba 12, 2015.
Maiti zikiokotwa katika mitaa ya Bujumbura asubuhi ya Desemba 12, 2015. © REUTERS/Jean Pierre Aime HarerimanaTEMPLATE OUT

Baadhi ya wafuasi wa chama tawala walishambuliwa na kunyanyaswa na watu ambao hawakuweza kujulikana.

Kwa hofu ya kuuawa, maelfu ya wananchi wa Burundi, ikiwa ni pamoja wanaharakati wa haki za binadamu na wanasiasa wa upinzani, walikimbilia katika nchi jirani, hasa nchini Rwanda na Tanzania.

Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, zaidi ya Warundi 200,000 wameitoroka nchi yao katika kipindi cha miezi 19 iliyopita.

Ofisi ya shirika la Haki za Binadamu la Ligue ITEKA, Bujumbura, Burundi.
Ofisi ya shirika la Haki za Binadamu la Ligue ITEKA, Bujumbura, Burundi. © RFI/Sonia Rolley