DRC-SIASA

Utata kuhusu uraia wa Waziri Mkuu mpya wa DRC

Samy Badibanga, Waziri Mkuu mpya wa DRC, Septemba 1, 2016
Samy Badibanga, Waziri Mkuu mpya wa DRC, Septemba 1, 2016 JUNIOR D.KANNAH / AFP

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kumezuka utata kuhusu madai ya Waziri Mkuu mpya, Samy Badibanga, kwamba ana uraia wa Congo na wa Ubelgiji. Kwa upande wake Waziri wa Mahusiano na Bunge, amesema hali hii ya uraia wa Congo na Ubelgiji kwa Waziri Mkuu ni tatizo la kisheria na kimaadili lakini kwa kiongozi wa upinzani, mjadala huu hauna nafasi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa hati iliyochapishwa nakurushwa hewani na mpinzani kwenye intaneti, Samy Badibanga ana uraia wa Ubelgiji aliopewa mwaka 1992. Itakumbukwa kwamba, Katiba JAmhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaeleza kwamba uraia wa Congo hauendani sambamba na uraia wa kigeni kwa mtu ambaye anashikilia wadhifa serikali. Mtu yeyote mabaye anashikilia wadhifa serikalini anapaswa kuwa na uraia wa Congo, Katiba ya Congo inabaini.

Hata hivyo, licha ya Waziri wa Mahusiano na Bunge, Tryphon Kin-Kiey, ambaye alianzisha utata huo, mwishoni mwa wiki iliyopita, kuhusu uraia wa Waziri Mkuu mpya, swala hili linaoneka kuwa tatizo la kisheria na kimaadili.

"Waziri Mkuu aliyeteuliwa ni mtu muhimu kwetu sisi ambao ni kutoka katika kundi la walio bungeni. Ni rafiki, Mtu muhimu sana, lakini hapo sasa, kuna tatizo. Naona hali hii huenda ikakwamisha hali ya mambo nchni hapa. Anatakiwa kujiondoa katika uraia wa kigeni aliopewa. Kile Mimi najua haitakua rahisi kwenda hatua ya kula kiapo kama swali hili litakua halijapatiwa ufumbuzi. Swala hili ni tatizo kisheria na kimaadili. Huwezi kutetea maslahi ya Congo wakati una uraia mwingine. Ni kwa Bw. Badibanga kuchukua uamuzi, kuanzia sasa ili kutatua hali hii, " amesema Tryphon Kin-Kiey.

Samy Badibanga aliteuliwa Novemba 17, kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akichukua nafasi ya mtangulizi wake Matata Ponyo, aliyejiuzulu kufuatia makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo kati ya serikali na upinzani uliyoshiriki mazungumzo.