NSA-SIASA-FILLON

François Fillon ashinda katika kura za mchujo

François Fillon ameshinda uteuzi wa chama cha Republican nchini Ufaransa, kuwania urais mwaka ujao. Bw Fillon alikua akishindana katika kura hizo za mchujo dhidi ya Alain Juppé .

Fillon Juppé wakipeana mkono kwenye makao makuu ya Mamlaka kuu ya kura za mchujo za chama cha mrengo wa kulia, Novemba 27, 2016.
Fillon Juppé wakipeana mkono kwenye makao makuu ya Mamlaka kuu ya kura za mchujo za chama cha mrengo wa kulia, Novemba 27, 2016. ©REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo Mkuu wa zamani alimshinda mpinzani wake Alain Juppé katika kura ya mzunguko wa pili iliyopigwa siku ya Jumapili na kupata ushindi wa asilmia 67.

Baadaye ya ushindi huo, Fillon ameahidi kujenga jamii yenye usawa na amesisitiza kuwa, Ufaransa inataka ukweli na vitendo.

Bw Juppé aliyepata asilikia 33 amempongeza Fillon kwa ushindi na sasa anatarajiwa kumenyana na mgombea wa chama cha Kisosholisti pamoja na Marine Le Pen kutoka chama cha National Front.

Uchaguzi wa urais utafanayika mwezi Aprili mwaka ujao.